Friday, 26 April 2019

WAZIRI WA NISHATI DKT. MEDARD KALEMANI AZINDUA UMEME VIJIJINI KATIKA WILAYA YA KITETO

WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani ameendelea kuzindua miradi ya umeme ikiwa ni muendelezo wa kuunganisha umeme vijijini na safari hii ikiwa ni zamu ya vijiji vya wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Aprili 25, 2019 katika kijiji cha Dosidosi, Dkt. Kalemani alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Dkt. John Pombe Magufuli, kupeleka umeme katika kila kijiji nchini.
“Kupitia miradi inayoendelea ya umeme vijijini , utekelezaji huu unalenga kuifikia azma yaa Serikali ya kuwapatia umeme wananchi wote wa vijijini ifikapo mwaka
2025.” Alisema.
Akifafanua zaidi Dkt. Kalemani alisema kufikia Septemba mwaka huu wa 2019, vijiji vya Orgine, Soweto, ikiwa ni pamoja na vijiji vingine 74 vitaunganishiwa umeme.
Mhe. Waziri pia aliwaagiza mameneja wote wa TANESCO nchini kuhakikisha wanawaunganishia umeme wateja wote walio lipia hadi tarehe 31 mwezi Machi.
 “Gharama za kuunganisha umeme ni shilingi elfu 27,000 tu, hivyo natoa wito kwa wananchi tumieni fursa hii ya kufikiwa na umeme kwa kulipia koasi hicho cha fedha ili ufaidike na nishati hii katika kukuza uchumi wako na taifa kwa ujumla.” Alisisitiza.
Kwa upande wake, Mbunge wa Kiteto Mhe. Emily Papian alimshukuru Dkt.Ksalrmani kwa kuzindua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika jimbo la Kiteto pia kwa kutoa Vifaa vya Umeta 250 vitakavyogawiwa kwa wananchi ambao hawata weza kufanya “wirering”katika nyumba zao ili waweze kuunganishiwa huduma ya umeme.
 WAZIRI wa Nishati Dkt. Medard Kalemani(aliyevaa shati jeupe), akiwa na Mbunge wa Kiteto Mhe. Emily Papian (kulia), akizunhgumza na wananchi huku akiwa ameshika moja ya vifaa vijulikanavyo kama Umeta vilivyogawiwa kwa wananchi ambao hawana uwezo wa kuweka mfumo wa waya kwenye nyumba (wiring) ili kuunganisha umeme na badala yake watatumia vifaa hivyo. Hii ilikuwa ni wakati wa kuzindua huduma ya kuunganisha umeme kwenye baadhi ya vijiji vya wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Aprili 25, 2019.


Mhe. Dkt. Medard Kalemani akizungumza  na mafundi wanao endelea kuunganishia umeme wateja  wa Kijiji cha Osteti  kilichopo kata ya Chapakazi wilayani Kiteto Mkoani Manyara  , ambapo Mhe. Dkt Medard kalemani alizundua mradi wa umeme vijijini katika kijiji hicho leo 

No comments:

Post a Comment