Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa ushauri kwa Viongozi vijana waliopewa madaraka na kudharau wengine katika jamii.

Dkt. Kigwangalla amesema kuwa katika maisha yangu mafupi kwenye siasa za Kitaifa ameshuhudia wengine wakijiona wakubwa kuliko wakubwa zao

"Kuna vijana wakipewa madaraka ama wakitajirika basi hubadilisha tembea/sema yao, dharau inatamalaki na hata husahau walikotoka. Katika maisha yangu mafupi kwenye siasa za kitaifa nimewashuhudia wengine hata wakijiona wakubwa kuliko wakubwa zao. Nawasihi wajifunze kwa Luqman," ameandika Waziri Kigwangalla kupitia ukurasa wake wa Twitter.

"Luqman, Mwenye busara, ni Mtakatifu wa Mungu tunayesoma mafundisho yake kwenye Sura ya 31 ya Qur’an. Humo anamfundisha mwanaye, ‘usitembee juu ya ardhi ya Mwenyezi Mungu kwa Maringo’ maana ‘hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala kufikia urefu wa milima’. Nyenyekea. Acha Kibri."
Share To:

msumbanews

Post A Comment: