Monday, 15 April 2019

WAZIRI JENISTA KATIKA HAFLA YA KUZINDUA TAARIFA YA UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza wakati wa hafla ya kuzindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) iliyofanyika Jengo la Takwimu tarehe 13 Aprili, 2019 Jijini Dodoma.

Waziri Jenista akizindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey). (Kushoto) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko, Naibu Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Harusi Said Suleiman. (Kulia) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Dawa za Kulevya, Mhe. Osca Mukaza

Naibu Waziri wa Afya, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar  Harusi Said Suleiman akieleza namna Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar zimekuwa zikishirikiana katika kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Bara (TACAIDS), Dkt. Leonard Maboko akitoa maelezo mafupi kuhusu utafiti huo uliofanyika juu ya Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017.

Baadhi ya washiriki wakisikiliza hotuba ya Waziri Jenista (hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) iliyofanyika Jengo la Takwimu tarehe 13 Aprili, 2019 Jijini Dodoma.

Jenista akiwa pamoja na viongozi wengine wakifuatilia ripoti fupi iliyokuwa ikiwasilishwa na mwakilishi kutoka Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) hayupo pichani. (Wa pili kutoka kushoto) ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri anayeshughulika masuala ya Watu wenye Ulemavu Mhe. Stalla Ikupa.

Jenista akionesha kitabu cha Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) baada ya kuzindua taarifa hiyo, Jijini Dodoma

Jenista akimkabidhi kitabu cha Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) Dorothy Mwaluko mara baada ya Kuzindua taarifa hiyo, Aprili 13, 2019 Jijini Dodoma.

Jenista akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi na wadau wa maendeleo mara baada ya kuzindua Taarifa ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya Ukimwi wa Mwaka 2016 – 2017 (Tanzania HIV Impact Survey) Jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment