Monday, 22 April 2019

WAWILI WAFARIKI AJALI ODONYOSAMBU ,WANANCHI MSIANDIKE VITU AMBAVYO AMNA UHAKIKA NAVYO

 Mkuu wa wilaya ya Arumeru  Ndugu Jerry Cornel Muro akizungumza na Mganga mkuu wa Halmashauri ya Arusha Dc Dokta  Petro  Mboya mara baada ya kutoka kuwatembelea majeruhi wa ajali  iliyotokea Odonyosambu.

Watanzania wametakiwa kuacha kukurupuka na kuandika vitu  ovyo na zinazozua taaruki pindi   tatizo linapotokea badala yake  wasubiri taarifa kutoka maamlaka husika.

Hayo yamesemwa leo na  mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kuwatembelea majeruhi wa ajali ya gari iliotokea  jana  katika eneo la Odonyosambu jijini hapa .

Ambapo mkuu huyo wa wilaya alianza kwa kukanusha taarifa ambazo zinasambaa ovyo mitandaoni na sehemu mbalimbali zinazodai kuwa katika ajali iliotokea jana watu nane wamefadiki duniana watu hao ni wa nchi jirani ya Kenya  kitu ambacho sicho cha kweli kwani katika ajali hiyo watu wawili tu ambao majina yao hayajatambulika ndio wamefariki dunia 

Aliwataka wananchi waache kusambaza  na kuandika taarifa ambazo zinazua taaruki na zinasumbua watu mbalimbali ambao wanataka kujua kitu ambacho kinaendelea 

"sisi tumefika tumejirizisha miiili tulioipokea ni miili miwili tu ,na majeruhi ni wanne na baadhi ya ndugu wa majeruhi kutoka nchi jirani wapo hapa wanaangalia ndugu zao na pia hata hawa majuruhi wa hapa nchini pia wapo hapa wanawaangalia najitiada za kunusuru maisha yao zinaendelea na sisi kama serikali  tunapambana kuhakikisha kila linalowezekana kuokoa maisha yao "Alisema Muro

Aidha aliwataka wananchi wa Arumeru na mkoa wa Arusha kwa ujumla  iwapo watataka kufanya matukio yeyote yale kama  kusanyiko lolote linalolenga shughuli za pembezoni ya barabara  lazima tukio hilo liripotiwe kwa serikali ili serikali iwaandalie vitu vya usalama na watu waache kufanya vitu kwa mazoea kwani  serikali hii haiendeshi kwa  mazoea bali kwa kufuata sheria 

kwa upande wake mganga mkuu wa hospitali ya halmashauri ya Arusha Petro Mboya akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa wamepokea miili miwili  ya marehemu ambayo  bado majina yao hayajatambulika pamoja na  majeruhi wa nne  ambao kati yao mmoja yupo katika hali mbaya kwani aliumia zaidi  katika maeneo ya kichwa.

"hospitali yetu ya Selian lutheran hospital tumepokea majeruhi wanne ambao wametokea katika ajali iliyotokea oldonyosambu  na katika hao wanne wawili wameumia vichwa na wapo chumba maututi mmoja ameumia uti wa mgongo ili huyu mmoa aliyeumia kichwa sana tumempa rufaa ya kwenda kumuona daktari bigwa wa mfumo wa fahamu,pia tulipokea maiti mbili ambazo tumeziifadhi katika vyumba vyetu vya kuhifadhia maiti hapa hapa hospitalini kwetu"alisema Mboya

No comments:

Post a Comment