Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2019 Mzee Mkongea Ali amekataa kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ya vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Kenswa kata ya Katumba na mradi wa ujenzi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilometa 0.64 katika kijiji cha Songambele yenye thamani ya shilingi milioni 289.747 katika halmashauri ya nsimbo wilaya ya mpanda; mkoani Katavi kufuatia kuwepo kwa mapungufu kadhaa;

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru pia aliagiza kukamatwa kwa meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini wa wilaya hiyo mhandisi Manase Simtala kwa kuidanganya serikali


Hali hiyo imetokea mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa mbio hizo za mwenge zilibaini kutolingana kwa hesabu ya fedha zilizotumika kiasi cha shilingi 550,886 zilishinnwa kubainishwa matumizi yake kati ya milioni 40 zilizotumika katika mradi huo wa vyumba vya madarasa

Katika hatua nyingine watumishi 27 wa ngazi mbalimbali za halmshauri hiyo walijikuta wakiwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa muda wa takriban dakika 30 baada ya kukosa nidhamu; na kudhubutu kuendelea kukaa katika viti wakati risala ya utii ikisomwa
Share To:

msumbanews

Post A Comment: