Saturday, 13 April 2019

WASHEHERESHAJI(MCs) NCHINI WAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI DODOMA,WAJIPANGA KUFANYA MAAJABU.


Chama cha Washehereshaji Nchini Tanzania kwa kauli moja wamempongeza Mh Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwatumikia watanzania na kuamua kujenga Chuo na makao yao Dodoma katika kuenzi jitihada za Rais Magufuli na pia kutengeneza fursa zaidi za Ajira kupitia fani ya ushehereshaji.

Hayo yamesemwa jana mbele ya Naibu Waziri wa Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde  wakati wa ufunguzi wa Semina na Mkutano mkuu wa Chama hicho ambapo Washereshaji hao wameonesha dhamira yao ya kuifanya fani hii kuendeshwa kwa uweledi wa juu kwa kufungua Chuo rasmi cha Mafunzo kwa lengo la kutengeneza Fursa zaidi za Ajira.

“Tumedhamiria kuipa heshima fani hii,Serikali mtuunge mkono kwa maana Fani hii hivi sasa inatoa Ajira za kutosha kwa Watanzania wengi.Tutajenga Chuo Dodoma pamoja na Makao makuu,Tunakushukuru Mh Mavunde kwa kutusaidia upatikanaji wa kiwanja na mchango wa mifuko 100 ya saruji”Alisema MC Makena-Mwanzilishi wa Chama cha Washereheshaji

Akifungua semina hiyo,Naibu Waziri Mavunde amepongeza kwa mpango mzuri ulioainishwa na Chama na kuahidi kwamba Serikali itatoa ushirikiano wa kutosha kwa kuwa inatambua vyema kwamba fani hiyo inatoa Ajira za kutosha.

Mavunde pia alitumia fursa hiyo kuwataka Washereheshaji hao kuhakikisha wanalipa kodi ili wachangie katika maendeleo ma ustawi wa Taifa Tanzania.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA.

No comments:

Post a comment