Na Humphrey Shao , Globu ya Jamii
Tasisi ya Utafaiti na sera nchini (REPOA) Itafanya Warsha ya Mwaka kwa watafiti kote nchini na kutoika mataifa mbalimbali Duniani kwa muda wa siku mbili kuanzia April 10 Mpaka 11 katika ukumbi wa Ledger Plaza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mtendaji wa REPOA, Dk. Donald Mmary amesema kuwa katika washa hiyo ambayo itahusisha mada kuu isemayo 'MAENDELEO YA UCHUMI WA NDANI KATIKA NGAZI YA CHINI' kama njia kuharakisha mapinduzi ya kimaendeleo nchini Tanzania ambapo katika mapinduzi hayo watazungumzia mapinduzi ya kilimo na viwanda.
“Nchi yetu imepiga hatua kubwa kulingana na uchumi kukua lakini bado kuna maeneo yanayogusa wananchi kuonekana hayajabadilika kwa kasi kwahiyo wameamua kuliangalia hilo jambo hasa ukuaji wa uchumi katika ngazi ya chini kuanzia ngazi ya almashauri, vijiji, mitaa na jamii kiujumla”. Amesema Dk.Mmary.
“Tunatambua kwamba tunapozungumzia maendeleo ya maendeleo ya ndani kwa ngazi ya chini tunazungumzia uwezo wa kutambua fursa zilizopo ambazo zinatokana narasilimali zilizopo hapa nchini”. Amesema Mmary.
amesema kuwa, ukiachana na suala la kutambua fursa vilevile kunakutafuta mbinu na mikakati ya kuzigeuza hizo fursa baada ya kuzitambua na kuwa katika shughuli za kiuchumi.
Pamoja na hayo kiongozi huyo ameongeza kuwa katika washa hiyo wanaweza kujifunza kutokana na uzoefu ambao viongozi mbalimbali wamepata ndani ya nchi kuona changamoto ziko wapi, tunaelekea wapi na tunakosea wapi.
“Tunatambua kwamba nchi yetu ni kubwa na inavigezo vyote vya saizi na ukubwa wa idadi ya watu kulingana na nchi nyingine za Afrika”. Mmary ameongeza.Kwa upande wake mkurugenzi wa tafiti za kimkakati, Jamal Msami amesema kuwa watakuwa na wawasilishaji wa mada kumi na pia kutakuwa na majukwaa ya kujadili muunganiko wa uhusiano katika mada na sera za maendeleo ambapo huko kutakuwa na wataalamu mbalimbali ambao wanaweza wakawa wajasiliamali, viongozi, wabobezi wa mambo ya taaluma za elimu, ujasiliamali na masuala ya uwekezaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Dkt. Donald Mmary akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Kongamano hilo kutoka REPOA Dkt. Jamal Msami akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam
Baadhi ya Waandishi wa Habari walioshiriki Mkutano huo wa REPOA wakimsikiliza Dkt. Donald Mmary
Share To:

Post A Comment: