Sunday, 21 April 2019

TANGA UWASA YAANZA MCHAKATO WA KUSAKA WAFADHILI KWA AJILI YA KUJENGA MIUNDOMBINU YA MAJI TAKAMAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) ipo kwenye mchakato wa kutafuta fedha kwa wafadhili kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kutibu maji taka.

Hayo yalisema hivi karibuni na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa, Mhandisi Geofrey Hilly ambapo alisema wameamua kufanya hivyo kwa sababu hivi sasa wanayamwaga baharini bila kuwepo kwa matibabu yoyote.

Mkurugenzi huyo alisema hivi karibuni alitoka wizarani kufuatilia andiko lao na kwamba linaendelea vizuri ambapo tayari limekwisha kunadiwa kwa wafadhili mbalimbali litakapo fanikiwa kabla ya mwaka huu haujaisha watapata mfadhili ambaye atawafadhili kujenga miundombinu hiyo.

“Mfumo wa maji taka bado hatupo vizuri lakini tupo kwenye mchakato kutafuta fedha kwa wafadhili kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kutibu maji taka kwa sababu kwa sasa tunayamwaga baharini bila ya kuwa na matibabu yoyote”Alisema

“Lakini sisi Tanga Uwasa kupitia uwezo wetu wa ndani kujenga mifumo inayoitwa disentrolize system unachukua block kadhaa za nyumba unatengenezea mfumo wake wa maji taka hiyo wanataka kuifanya kwa uwezo wa ndani hususani maeneo ya pembeni ambayo hayawezi kuunganishwa kwenye mtandao mkuu uliopo sasa”Alisema

Hata hivyo alisema hivi sasa wanajipanga kujenga miundombinu na kuongeza mabomba zaidi ya kilomita 100 za mabomba ya maji taka ili kuimarisha utoaji wa huduma ya maji taka.

Mwisho.

No comments:

Post a comment