Katibu wa Chama Cha Mapinduzi mko wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka amesema  Watanzania hawataacha kusahau wala kughafilika katika suala la kumuenzi, kumuheshimu na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa katika taifa hili na Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hayati Sheikh Abeid Amani Karume

Amesema ndiye kiongozi pekee aliyekuwa na uthubutu wa kuiunganisha nchi yake na kuunda Jamhuri moja ya Muungano na kuzaliwa kwa Taifa jipya liitwalo Tanzania.

 Shaka aliyasema hayo jana wakati akizungumzia kumbukumbu ya miaka 47 ya kifo cha hayati Mzee Abeid Amani Karume amesema kiongozi huyo alikuwa shujaa, mzalendo, mpigania haki na mpenda umoja wa Afrika na watu wake.

"Maisha ya hayati  Karume kushiriki kwake siasa, kutumia muda mwingi kukijenga Chama Cha ASP hadi kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar na kupatikana ukombozi kamili wa waafrika Zanzibar,  kuna mchango mkubwa wa hekima, busara na ujasiri wa kiongozi huyo, daima milele tutaendelea kumuenzi sheikh Karume ,kujifunza kutokana na ushupavu wake lakini pia maono yake ya mbali katika kupigania maendeleo na usawa wa kila mtu,

"Viongozi wengi katika Afrika wakati wa kupigania uhuru walionekana kuahidi kuwa wataungana baada nchi zao kupata uhuru ili kuifanya Afrika kuwa moja, wote walishindwa ila walioweza ni Mwalimu Julius Nyerere na sheikh Abeid Amani Karume "aliongezea Shaka

Shaka alisema hayati  Karume ndiye aliyemwambia Mwalimu Nyerere   waungane  haraka na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere awe Rais wa kwanza   wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jambo ambalo lilihitaji ujabali, ujasiri na uzalendo wa kutosha ili kufikia maamuzi magumu ambayo yanakwenda kulijenga na kulimairisha Taifa bila ya tamaa ya aina yoyote.

"Walipokubaliana kuziunganisha nchi zao mbili huru , Mzee Karume hakutaka longolongo, alimueleza Mwalimu Nyerere tukawaulize wananchi ili tuungane, akasema Rais wa kwanza wa muungano uwe wewe Mwalimu Nyerere, uamuzi huu viongozi wengi Afrika uliwaishinda kwa tamaa ya madaraka "Alisiaiatiza Shaka

Hata hivyo Shaka amefafanua kuwa jukumu la kila Mtanzania kwa sasa ni kuendelea kuamini kuwa kilichokufa mwaka 1972 ni kiwiliwili cha sheikh Karume bali fikra na mema yote alioyaanzisha katika uhai wake yanadumishwa kinadharia na vitendo na siku zote kuendelea   kuamini  kuwa, njia pekee yenye heshima, utii na upendo ni kuyatetea mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 1964 na kuilinda misingi ya Muungano wa April 1964 bila kughilihiwa na kifikra au njama za vitimbakwiri wasiolitakia mema Taifa.

Source Mtanzania
Jumapili 7 April 2019
Share To:

msumbanews

Post A Comment: