Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejizatiti katika kuondosha tatizo la Uhaba wa madarasa katika shule za msingi na sekondari Zanzibar.


Alisema kwa kipindin kirefu wanafunzi shule za msingi na sekondari wamekuwa wakikabiliwa na changamoto hiyo ya madarasa kuwa madogo hivyo serikali imejipanga katika kuwaondolea changamoto hiyo.

Hayo aliyasema wakati akizungumza na kamati za Skuli za Sekondari za Mahonda na Fujoni pamoja  na Walimu wakati wa ziara  ya kukagua Kumbi mbili za kufanyia Mitihani za Shule  hizo zilizojengwa kwa nguvu za Wananchi na Walimu



Alisema moja ya mmango uliopagwa na serikali katika kuhakikisha wanaondokana na changamoto hiyo ni utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa majengo mapya ya shule za sekondari za ghorofa unaofanywa hivi sasa ambapo kukamilika kwa mradi huo utaondosha changamoto hiyto.


Balozi alisema Mradi huo uliopangwa kutekelezwa kwa Shule zipatazo 20 kila Wilaya pamoja na yale maeneo yenye idadi kubwa ya Wanafunzi wa Sekondari italeta faraja kubwa mbali ya Wanafunzi lakini pia kwa Wazazi.

Pia alisema Alisema Serikali Kuu kupitia Sera ya Elimu ililazimika kujizatiti katika kuongeza Majengo ya Skuli kwa lengo la kukidhi mahitaji halisi ya ongezeko kubwa la Idadi ya Watu Nchini ambayo asilimia kubwa ni Wanafunzi.

Balozi Seif  alisema wakati Serikali ikiendelea na harakati zake za kujenga miundombinu katika Sekta ya Elimu, Uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania {Tasaf } unaoratibiwa na Ofisi yake kwa upande wa Zanzibar umeahidi kuongezea nguvu Miradi iliyoanzishwa na Wananchi.

Alisema Tasaf Awamu ya Tatu katika mkupuo wa Pili imejipanga kukamilisha ujenzi wa Kumbi Mbili za Mitihani za Skuli ya Mahonda na Fujoni ambazo zimesita ujenzi wake kwa muda mrefu sasa.

“ Nakuthibitishieni Uongozi wa Skuli ya Sekondari Mahonda na Fujoni kukamilishwaujenzi wa Majengo hayo ili kuunga mkono nguvu za Wananchi zinazoonekana kutaka kupotea”. Alisema Balozi Seif.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: