Sunday, 21 April 2019

RC Ayoub aomba ushirikiano kwa Taasisi za kiserikaliNa Thabit Hamidu,Zanzibar.

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Ayoub Muhamed Mahmoud amewataka baraza la Manispaa Zanzibar, Halmashauri za Wilaya na Mabaraza ya Mji kufanya kazi kwa Mashirikiano ili kutimiza malengo ya Taasisi zao.

Ayoub alisema Taasisi hizo zinapofanya kazi kwa pamoja hupelekea kazi kufanyika kwa kasi na kuwa kichocheo cha maendeleo Nchini.

Hayo aliyasema wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Tatu wa Jumuiya inayoundwa na Taasisi hizo tatu, Halmashauri za Wilaya, Mabaraza ya Miji na Mabaraza ya Manispaa Zanzibar (J-SMZ), Uliofanyika katika Ukumbi wa Manspaaa ya Magharib A,Unguja.

Ayoub Alisema ni lazima kwa taasisi hizo kufanya kazi kwa mashirikiano ili kuongeza ufanisi na kazi ya kuleta maendeleo kwa wanachi.

“Ili mufanye kazi kwa kuzingatia Maslahi ya wanachi bila shaka hamuna budi ya kufanya kazi kwa mashirikiano katika taasisi zenu”RC Ayoub alisema.

Pia alisema iwapo watazingatia lengo la kuanzishwa kwa jumuiya hiyo ya pamoja, basi mashirikiano na kasi ya utendaji wa kazi utaongezeka na kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

“Najua kuna changamoto ambazo zinawakabili katika utendaji kazi wenu ila kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa mashirikiano ambapo mutatekeleza majukumu yenu ipasavyo”alisema Rc Ayoub.

Hata hivyo waliambia kupitia kwa jumuiya hiyo wananafasi kubwa ya kuchochea kasi ya maendeleo ya Nchi kutokana na Jumuiya kuwa daraja linawaunganisha na Serikali katika majukumu yao.

“Iwapo mtakipa umuhimu chombo hiki kwa kuwajibika kikamilifu kama katiba yenu inavyoelekeza, kitasaidia kupatikana kwa fursa mbali mbali za kustawisha maendeleo ya maeneo yenu jamii kwa ujumla”, alisema Ayoub

No comments:

Post a Comment