Na Rahel Nbali, Tabora.

Watu watano  wa  kijiji cha Isongwe  kata ya Mkolye Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora wa  familia moja wameuawa na watatu kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi  iliyoambatana mvua kubwa  ya upepo  iliyonyesha kijijini hapo.

 Methew sipemba ni Kaimu mganga mfawidhi wilaya ya Sikonge amesema alipata tarifa toka polisi juu ya tukio hilo na kukuta watu watano walisha poteza maisha.


“Ajali ya radi sio nzuri nikama moto watu hawa wamejikuta wanavuta hewa ya halufu kali na kuunguza mapafu jambo ambalo limepelekea kupoteza maisha” Amesema Sipemba .

kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kamishna msaidizi Emmanuel Nley Mvua amesema mvua hiyo ilisababisha ukuta wa Nyumba waliyokuwa wamelala familia  hiyo kupasuka  na kusababisha Vifo hivyo.

“Nyuma ilikuwa imejengwa kwa udongo na makuti na kuezekwa kwa nyasi mvua iliponyesha ilisababisha ukuta kupasuka na kupelekea tukio hilo kutokea” Amesema Nrey.


Nrley amesema Katika tukio hili walio poteza maisha ni pamoja na Mhindi Peter, Vailet Juma ,gress juma, kuluwa lukanya na Nyanzobe juma.

Tukio hili  llimeibua simanzi miongoni mwa wanannchi Peter Nzalalila ni mwenyekiti wa halimashauri ya wilaya ya sikonge amewataka wananchi wa eneo hilo kuacha kuhusisha tukio hili na imani za kishirikina .

“Nawataka wananchi kuacha kuhusisha tukio hili na imani za kishirikina  Serikali halita fumbia macho kwa mtu yeyote atakaye vunja sheria”Amesema Nzalalila.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: