Saturday, 27 April 2019

Prof. Ndalichako akagua hatua za maandalizi ya uwekaji wa Jiwe la msingi chuo cha Mzumbe

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako leo ametembelea na kukagua hatua za maandalizi ya ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Mbeya, ambapo amepongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Mzumbe kwa hatua za ujenzi ulipofikia.

Akiwa ameambatana na Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Pro. Lughano Kusiluka, Prof Ndalichako amemwelekeza Mkandarasi wa Ujenzi kuhakikisha kufikia Juni 2019  ujenzi wa Jengo hilo kuwa umekamilika kama ilivyopangwa.

Kukamilika kwa ujenzi kutawezesha jumla ya wanafunzi 900 kupata vyumba vya madarasa mbali na kumbi za mikutano na ofisi za uendeshaji. 

Jengo hilo linatarajiwa kuwekwa jiwe la Msingi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Joseph Magufuli Mei 1, 2019.

No comments:

Post a Comment