Thursday, 18 April 2019

POLEPOLE AAGIZA KAMATI ZA SIASA ZA KATA KUINGIZA AJENDA ZA MAENDELEO.

Na EZEKIEL MTONYOLE, DODOMA.
KATIBU wa itikadi na uenezi wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Hamphrey Polepole ameagiza katika ufunguzi wa kamati za siasa za kata kuweka ajenda za maendeleo  ambazo zitahusisha wataalam wa eneo  ili kueleza hali halisi ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa makatibu waenezi wa kata zote na kamati za siasa za mkoa wa Dodoma, ikiwa ni kutekeleza mkakati wa kukuza na kukomaza Demokrasia mashinani.

Polepole amesema kuna haja ya kamati zote za siasa za kata  kabla ya kuanza vikao vyao kuweka ajenda za maendeleo na waweke maada ya kujadili maendeleo na ihusishe wataalamu na viongozi wote  wa kata hizo kueleza nini serikali imefanya au inafanya  katika maeneo  yao.

Amesema waeleze vitu au miradi ambayo inaendelea kutekelezwa na serikali, amesema wataalamu waeleze kama kuna miradi kama daraja, makaravati au fedha iliyoletwa na serikali ni shingapi na itafanya nini katika maeneo yao ili wananchi wajue serikali ambayo miradi inaitekeleza.

Amesema wao kama chama cha mapinduzi ni sauti ya umma, kunahaja ya wao kupaza sauti kueleza, badala ya kuziachia asasi za kiraia kuisemema ambapo mara nyingi hupotosha ukweli,  hivyo nafasi hiyo ichukuliwe na CCM, kupaza sauti.

Amesema kuna bilioni mia tano zimetengwa kwa ajiri ya  kujenga barabara za mzunguko katika makao makuu, barabara mia moja jijini Dodoma ikiwa ni fadhila kwa kuwa ngome ya chama cha mapinduzi na kushika viti vingi katika idara mbalimbali.

Amesema wataendelea na kuwatumikia wananchi na hawatakubali kuyumbishwa na  wapinzani, na wataendelea kuwa imara kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma Godwin Mkanwa, amesema katika uchaguzi uliopita walipoteza kata sita na kati ya hizo kata nne tayari zimerejea CCM, na bado kata mbili ambazo wanauhakika katika uchaguzi  ujao watashinda na kushinda kata zote.

No comments:

Post a Comment