Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Faustine Ndugulile, ameitaka jamii kuacha kuwaficha wagonjwa wa akili na badala yake amewataka wawafikishe katika vituo vya afya, ili waweze kupatiwa matibabu kwa kua ugonjwa huo unatibika.

Naibu Waziri ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma, wakati alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo, aliyetaka kujua Serikali ina mpango gani katika kuwatibia wagonjwa wa akili wanaolandalanda barabarani.

Naibu Waziri Dk. Ndugulile, amesema pamoja na uwepo wa sheria inayohusu magonjwa ya akili kuitaka jamii kuwapeleka watu hao katika vituo vya afya, kwenda kuwapatia matibabu, lakini jamii yenyewe hasa ndugu wamekuwa wakiwanyanyapaa, na mara nyingi wamekuwa wakihusisha ugonjwa huo na imani za kishirikina.

Tatizo hilo hivi sasa limetajwa kuongezeka huku chanzo cha magonjwa hayo kikiwa ni pamoja na msongo wa mawazo, kurithi na uvutaji wa vilevi mbalimbali.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: