Tuesday, 16 April 2019

Msanii Mwana FA akutana na Kocha Jose Mourinho


Kwa sasa msanii wa Bongo Fleva, Mwana FA anazungumziwa sana kwa upande wa michezo mara baada ya kuchapisha picha kwenye mtandao akiwa na Kocha Jose Mourinho.

Rappa huyo aliyejizolea umaarufu mkubwa kutoka na ngoma zake zenye tungo kali, ameeleza furaha yake mara baada kukutana na kocha huyo mbwatukaji.

"Nilifurahi kukutana na Jose Mourinho leo..yale maneno mabaya yote nikayaficha, nikamshukuru kwa nyakati nzuri alipokuwa kwetu na kumtakia bahati njema popote anapokwenda. Na kuwa mimi ni mshabiki wake mkubwa,hasa anapoanza kuchonga, i feel good kukutana na this great man!" ameeleza FA.


Utakumbuka hapo juzi, Jumapili Mwana FA alikuwa jijini Manchester nchini Uingereza kuishuhudia timu yake ya Man United wakati ilipowakabili wagonga nyundo West Hama United.

No comments:

Post a Comment