Sunday, 21 April 2019

MGOMBEA WA CCM JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI APITA BILA KUPIGWA


Mgombea wa  ubunge kwa tiketi ya chama cha  Mapinduzi  (CCM) John Daniel Pallangyo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa kuwa mbunge mteule wa Jimbo la Arumeru Mashariki. 

 Aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha Demokrasia Makini Simoni Paul Ngilisho akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kushindwa kukidhi vigezo na sheria vya Tume ya Uchaguzi Taifa 
Juma Mohameda  alikuwa mgombea kwa tiketi ya chama cha ADATADEA  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya chama chake kushindwa kutimiza sheria na taratibu zinazohitajika kufuatwa. 

Na. Vero Ignatus, Arumeru.

Aliyekuwa mgombea wa  ubunge kwa tiketi ya chama cha  Mapinduzi  (CCM) John Daniel Palangyo  amepita bila kupigwa katika uchaguzi mdogo wa jimbo la arumeru Mashariki.

Akimtangaza  Mbunge  huyo msimamizi wa  Uchaguzi Emanuel Mkongo  amesema kuwa hali hiyo inafuatia wagombea jumla ya wagombea 11 walichukuwa fomu ya kugombea ubunge wa jimbo hilo na wagombea Tisa wamerejesha fomu hizo huku wagombea watatu wakiwa hawajarejesha kabisa wengine  kushindwa kujaza fpp} kwa usahihi hivyo kukosa vigezo.

Mkongo amesema Baadhi ya wagombea hao ambao wameshidwa kukidhi vigezo ni pamoja na wagombea watatu ambao hawakuteuliwa kwasababu hawajarudisha fomu ,huku wengine wakiwa saba wakiwa wamerejesha lakini hawakukidhi pamoja na kutolipa dhamana ya kugombea   ubunge  ambayo ni shilingi elfu 50 wadhamini pamoja na kuleta hati ya kula kiapo kutoka kwa mwanasheria na hakimu.

Msimamizi huyo wa uchaguzi amesema kuwa katika fomu hizo fomu moja tu ndio ambayo ilikuwa haina mapungufu ya kisheria hivyo alitumia  nafasi hiyo kumtangaza John Pallagyo  kupita bila kupigwa na kuteuliwa kuwa mbunge Wa jimbo la Arumeru mashariki .

Kwa upande wake mgombea wa chama cha Demokrasia Makini Simoni Paul Ngilisho amesema kuwa jambo kubwa lililosababisha chama chake kushindwa katika kuchukua nafasi ya ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki ni  kwamba wananchi hawana imani nao hivyo  kupelekea kukosa wadhamini 31 ili kukamishisha sheria ya NEC.

 Nae Juma Mohameda  mgombea wa chama cha ADATADEA amesema alitekeleza matakwa yote ya kisheria na akaridisha fomu lakini zikagundulika zinamakosa, hivyo amesema watashirikiana na mbunge mteule aliyeteuliwa wa CCM kwaajili ya shughuli za maendeleo Jimbo la Arumeru Mashariki

Nitajipanga kwa awamu ya mwisho 2020 ili kuhskikisha chama changu kinapata nafasi ya kuongoza katika jimbo hili. Alisema Mohamed

Akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi Pallagyo amesemaa anawashukuru viongozi wake wa chama kumpitisha katika ngazi ya wilaya hadi Taifa.

Amesema atashirikiana na viongozi wenzake na viongozi wa jimbo kuhakikisha kuwa wanaondoa kero ambazo wananchi wamekuwa wakizipitia

Amesema jimbo hilo limekuwa nje ya mfumo kwa muda mrefu  1995 kwa muda wa miaka 5,mtu wa kusemea matatizo ya eneo husika alikuwepo kutoka NCCR lakini hakuonekana tangia alipochaguliwa, 2012 hali ikaendelea kuwa mbaya, 2015, kwa baraka hizi nitajitahidi nitamlilia mhe. Rais, hatuna barabara king'ori kwenda Leguruki,Akeri,  maji-Malula, siku Rais alikuja kutuomba kura alituahidi km 5 za lami tutaanzia hapo. Alisema Pallagyo. 

No comments:

Post a Comment