Thursday, 18 April 2019

Manispaa ya Ilala kugawa kadi za Wazee za matibabu

Kaimu Meya wa Manispaa ya Ilala Omary Kumbilamoto alimkabidhi shilingi Milioni 3.1Mweka hazina wa Jumuiya ya Wazee wa Kata ya Ukonga Ally Jumaa Dar es Salaam leo,kwa ajili ya Kuendesha shughuli za biashara ya jumuiya ya Wazee Ukonga (Kulia) Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Joyce Maketa na Diwani wa Ukonga Jumaa Mwaipopo.

Na Heri Shaaban 
MANISPAA ya Ilala Dar es Salaam inatarajia kuwapiga picha za vitamburisho vya bima ya afya kwa wazee wa Manispaa ya Ilala. 

Mpango huo ambao unatatibiwa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo kupitia Idara ya Ustawi wa Jamii Ilala. 

Akizungumza Dar es Salaam leo wakati wa kutoa Msaada kwa kikundi cha Jumuiya ya Wazee wa Kata ya Ukonga Kaimu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto alisema jumla ya kata 24 za Ilala zinatarajia kupatiwa vitamburisho hivyo vya Wazee. 

"Idara ya Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala kupitia Ofisi ya Mganga Mkuu awamu ya kwanza ilifanikisha kuwapatia Wazee kadi za matibabu 7699  kata 34,awamu ya Pili Wazee 5606 kutoka kutoka Kata 15 bado kata 24 mpango huu endelevu unaendelea  mwezi Aprili mwaka huu "alisema  Kumbilamoto. 


Kumbilamoto alisema  awali zoezi hilo lilifanyika katika Kata mbalimbali za Manispaa ya Ilala pia baadhi ya kata Wazee wanarudiwa tena kupigwa picha waweze kupewa kadi zao.

Akizungumza na Wazee wa Jumuiya ya Ukonga Kaimu Meya Ilala,alisema  wamewapa mtaji wa Shilingi milioni 3.1  ili waweze kujishughulisha na shughuli mbalimbali. 

Amewataka wazee wa Jumuiya hiyo kuendeleza Umoja wao ili waweze kufikia Malengo waliokusudia. 

Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala Joyce Maketa alisema mtaji huo waliopewa na Manispaa Ilala kwa ajili ya kununua meza, sufuria, viti, Maturubahi na sahani vitakuwa vinakodishwa na Jumuiya hiyo ya Ukonga. 

Joyce aliwataka wadau wa maendeleo kujitokeza idara ya ustawi wa jamii Ilala   
Kusaidia vikundi mbalimbali vilivyopo chini ya idara hiyo. 


Naye Mweka hazina wa Jumuiya ya Wazee wa Kata ya Ukonga Ally Jumaa alipongeza msaada huo walipewa na Manispaa Ilala watatumia kwa malengo yaliyokusudiwa. 


Jumaa alisema Jumuiya hiyo ilianzishwa mwaka 2006 idadi yao katika Jumuiya wapo 2000 kati yao 500 walishapewa kadi za matibabu changamoto wakiumwa nauli za kwenda kufuata matibabu hawana. 

Diwani wa kata ya Ukonga Jumaa Mwaipopo alisema yeye ni Mlezi wa Jumuiya hiyo ipo ndani ya Kata yake. 

Mwisho

Aprili 17/2019
Ukumbi wa mikutano Arnatoglou

No comments:

Post a Comment