Thursday, 25 April 2019

Makosa makubwa ya jinai 45,574 yaripotiwa Polisi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kang Lugola amewasilisha bungeni hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jumla ya shilingi Bilioni 921.

Katika hotuba yake Waziri Lugola ameeleza kuwa katika kipindi cha mwezi Julai 2018 hadi Machi 2019 jumla ya makosa makubwa ya jinai 45,574 yaripotiwa katika vituo vya polisi ikilinganishwa na makosa 47,236 yaliyotokea katika kipindi kama hicho mwaka 2017/18.

Pia katika kipindi cha mwezi Julai 2018-Machi 2019 jumla ya matukio 2,593 yameripotiwa ikilinganishwa na matukio 4,180 yaliyoripotiwa kwa kipindi kama hicho mwaka 2017/18. Takwimu hizi zinaonesha kuwa matukio ya ajali yamepungua kwa asilimia 38.

No comments:

Post a Comment