NA VERONICA MWAFISI, MOHA

WAZIRI wa Mambo yaNdani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoawito kwa watumishi wa wake kitengo cha kushughulikia malalamiko ya wananchi, kutekeleza wajibu wao wa kufuatilia na kuyapatia ufumbuzi wa haraka malalamiko wanayopokea.
Lugola amesema hayo Jijini Dodoma juzi katika kikao kazi kilichoshirikisha watumishi wa kitengo hicho.
Amewataka wafuatilie malalamiko yanayotolewa na wananchi dhidi ya taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ambazo ni Jeshi la Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
“Hakikisheni malalamiko mnayoletewa, mnayapatia ufumbuzi wa haraka bila kufika ngazi ya juu, tekelezeni wajibu wenu kwa ufanisi ili kujenga imani kwa wananchi (walalamikaji).

“Kama  wananchi watajiridhisha kuwa kitengo hiki ni msaada mkubwa kwao,  mtakuwa mmejijengea uaminifu na kuifanya Wizara ijitegemee kushughulikia malalamiko,” alisema Lugola.

Lugola alisisitiza umuhimu wa viongozi wanaoshughulikia malalamiko yanayotolewa na wananchi kuchukuliwa hatua kama itabainika wameshindwa kutimiza wajibuwao.

Amesisitiza umuhimu wa kubadili mfumo wa kushughulikia malalamiko akisema yanapofikishwa katika kitengo hicho yachunguzwe hapohapo Wizarani.

“Malalamiko yasirudishwe kwenye taasisi zinazolalamikiwa kama Polisi, Uhamiaji, Magereza, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na  NIDA, pia walalamikiwa waitwe na kuhojiwa.

“Lengo ni kupata suluhisho la malalamiko yanayotolewa ili kuleta uhuru,  malalamiko yajibiwe kwa haraka na uwazi kwa njia ya barua au simu,  malalamiko ambayo yataonekana hayana ukweli walalamikaji wapewe taarifa,” alisisitiza Lugola.

Ameongeza kuwa,  malalamiko mengine hayapaswi kuchukua mudamrefu ili kutatuliwa akitolea mfano malalamiko ambayo aliyapokea kwa wananchi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka kwenye ziara alizofanya katika mikoa mbalimbali nchini.

Kwaupande wake, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu,  alitumia fursa hiyo kuwapongeza watumishi wa kitengohicho kwa kuyafuatilia malalamiko yanayotolewa na wananchi pamoja na kuyafanyia kazi kwa haraka.

Amesema kitendo cha kupokelewa,  kuyafanyia kazi malalamiko ya wananchi ndani ya muda mchache, kitawezekana kama kila mtumishi anayeshughulikia malalamiko atawajibika ipasavyo ili kupunguza mrundikano wa malalamiko yanayotolewa.

Ametoa wito kwa watumishi wa kitengo hicho kwenda maeneo mbalimbali ambayo yanamalalamiko ili kupata usahihi wa taarifa, kuzifanyia kazi na kutoa maamuzi.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara hiyo na kutoka Jeshi la Polisi, Magereza, Uhamiaji, NIDA na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: