Leo tarehe 17 Aprili, 2019 Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini imeanza kupewa mafunzo ya siku mbili kuhusu namna bora ya usimamizi wa mipango ya ushiriki wa watanzania katika Sekta ya Madini.

 Mafunzo hayo yanayoendelea katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Madini jijini Dodoma yanatolewa na Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara ya Madini, Edwin Igenge. Washiriki katika mafunzo hayo ni pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushiriki wa Watanzania katika Sekta ya Madini, Dkt. Athanas Macheyeki, Katibu wa Kamati hiyo ambaye ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Prof. Shukrani Manya, Mjumbe wa Kamati hiyo, Maruvuko Msechu, Mkurugenzi wa Ukaguzi na Biashara ya Madini wa Tume ya Madini,  Dkt. Venance Mwase.

Wengine ni pamoja na Mwanasheria wa Tume ya Madini, Salome Makange, Mwakilishi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini, Ringo  Irigo pamoja na wajumbe kutoka sekretarieti ya kamati hiyo.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA.







Share To:

msumbanews

Post A Comment: