Na Furaha John,Dodoma
WAKANDARASI waliopewa kazi ya kusambaza umeme katika Wilaya za Chamwino na Kongwa wametakiwa kuongeza kasi ya kusambaza umeme ili wananchi wote waweze kupata huduma hiyo muhimu.

Agizo hilo limetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Nishati, Merdard Kalemani wakati alipofanya ziara ya kikazi na kuwasha umeme katika shule ya Sekondari Buigiri na Kijiji cha Mwegamila wilayani Chamwino na Wilaya ya kongwa mkoani hapa.

Amesema, anafahamu kuwa kasi yao ya awali haikuwa ya kuridhisha mana ilikuwa ni ya kusuasua sana hivyo amelazimika kufika katika maeneo hayo ili kuongeza mkazo ili kasi ya kusambaza umeme iongezeke.

Kalemani amefafanua kuwa Tanesco kupitia mkandarasi hawana sababu ya kusuasua kuwasha umeme katika maeneo hayo kwa kuwa nguzo na nyaya wanazo za kutosha.

Waziri Kalemani, amewataka wananchi kulipia umeme ili waweze kuunganishia mara unapofika katika maendeo yao huku akimtaka Meneja wa Tanesco kuacha kukataa fedha za wananchi wanazotoa kwa ajili ya kuunganishiwa wanaohitaji umeme kwa kisingizio cha ukosefu wa vifaa mana jukumu hilo ni la mkandarasi.

Pia ametoa siku moja kwa mkandarasi kufunga nyaya kwenye nguzo ambazo hazina, kufunga mita na kuwaingizia umeme wananchi katika nyumba zao.

“Jambo la msingi na ninyi lazima mtumie umeme huu, kwa taarifa niliyonayo mkandarasi, mhandisi umeme haujaeneo jirani na vitongoji vya shule hii, kwa hiyo kwa anzia wiki ijayo ni mchakamchaka kuleta umeme katika vitongoji vilivyo jirani na shule hii,”alisema.

Akiwa katika mji wa serikali amemuagiza Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)mkoa wa Dodoma,Tumaini Nyari, kuongeza kasi katika kazi ya kusambaza umeme inayoendelea katika majengo ya wizara mbalimbali zilizopo katika mji huo.

Mbunge wa Chilonwa,Joel Mwaka aliomba, vitongoji vyote 11 vya kijiji hicho viwekwe umeme , sehemu ambayo itawafanya wananchi waweze kuvuta umeme kutoka kwenye maeneo hayo na kupeleka katika maeneo yao.

Katika ziara Wilayani Kongwa Waziri huyo, amesema, mpaka kufikia Juni mwaka huu vijiji 80 kati ya 87 vya wilaya ya Kongwa vitakuwa vimekamilika kupelekewa umeme.

Amesema kukamilika kwa vijiji hivyo katika mradi wa REA III, kutafanya asilimia 92 ya vijiji katika wilaya ya kongwa kuwa vimepata umeme.

Katika hatuna Nyingine amewataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kupeleka umeme katika vijiji 7 vilivyobaki katika awamu ya pili ya mradi.

Awali Mbunge wa Kongwa Job Ndugai, aliwataka wananchi kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za serikali za kuwapelekea huduma ya umeme kwa kutumia fursa hiyo kuingiza umeme katika nyumba zao.

Mbungebhuyo ambaye pia ni spika wa Bunge amesema, atashangazwa kuona katika chaguzi wanachagua chama ambacho hakijawapelekea maendelo ikiwemo nishati ya umeme na badala yake wakachagua ambacho hakijawapelekea maendeleo.

Aliishukuru serikali ya awamu ya Tano kwa jitihada kubwa inazozifanya kupeleka maendeleo kwa wananchi na kujali wananchi wanyonge na wenye hali ya chini.

Kwa Upande wake Meneja wa Tanesco Mkoa,alisema maagizo yote yaliyotolewa na waziri ameyapokea na atahakikisha yanafanyiwa kazi na kutekelezwa kwa wakati bila kusuasua.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: