Monday, 15 April 2019

Dc Katambi Aitaka Sauti ya Jamii Kuisaidia SerikaliMkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe Patrobas Katambi ameizindua rasmi rasmi taasisi ya Sauti ya Jamii na kuitaka kuisaidia Serikali katika kuleta maendeleo nchini.

DC Katambi ameitaka Taasisi hiyo kutumia rasimali watu wake katika kuwaelimisha wananchi mambo mazuri na makubwa ambayo yamekua yakifanywa na Rais Magufuli ambaye toka amekua Rais ametekeleza kwa kiwango kikubwa ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni.

" Nawapongeza sana Sauti ya Jamii nyie ni vijana ambao mmekua mkijitolea bila kulipwa kutembea Nchi nzima kumsemea Rais wetu Dk John Magufuli kwa watanzania mambo makubwa yaliyoyafanya ndani ya miaka mitatu, Miradi ya kimaendeleo kama Stiglers Gorge, Reli ya Kisasa ya umeme, Barabara za lami nchi nzima, amefufua shirika la ndege na kukomesha ufisadi ni baadhi ya mambo machache aliyoyafanya ndani ya muda mfupi," amesema DC Katambi.

Pia aliahidi kuwapa sapoti Taasisi hiyo katika kuwainua vijana wenye vipaji ambapo aliwakutanisha na mastaa wa filamu nchini, Rado, Niva, Man Fizo na Baba Haji ambao waliahidi kuwapa sapoti vijana hao.

Aidha ameitaka Taasisi hiyo kuendelea kushirikiana na Serikali na kuwaonya kutokubali kurubuniwa na wanasiasa ambao wamekua hawaitakii mema nchi yao.

No comments:

Post a comment