Shirika la Umeme  nchini Tanesco mkoani Arusha limefanya bonanza kubwa la michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu, mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku huku wadau wengi wakijitokeza kwenye viwanja vya General tyre  kushughudia michezo hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro amefungua bonanza hilo amesema kuwa michezo ni afya, ajira na furaha katika jamii hivyo bonanza hilo la Tanesco linalenga kuhamasisha wananchi kuunga mkono timu ya Vijana ya Taifa ya Serengeti ambayo inashiriki katika michuano ya Afcon.

Gabriel amesema kuwa michezo inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa yasiyoambukiza kama presha,kisukari na saratani ambayo husababishwa na aina ya maisha isiyozingatia mazoezi na lishe.

Kaimu Meneja wa Tanesco mkoa wa Arusha Donasiano Shamba amesema kuwa bonanza hilo linahusisha michuano mikali kati ya timu ya Tanesco na RAS arusha ambao walichuana katika mpira wa miguu na mpira wa pete.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: