NA HERI SHAABAN

CHAMA cha Mapinduzi CCM TABATA Mtambani kuwachukulia hatua Wajumbe wa Mashina walio shindwa kwenda na kasi ya Rais John Magufuli.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam leo na Katibu wa Tawi la Tabata Mtambani Ramadhani Kudunale wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu Tawi la Mtambani.

"Tulitoa maelekezo kama tawi tukiitaji Wajumbe wa Mashina mfanye vikao katika mashina yenu msikilize vikao  vya Wananchi pia mshirikishe Serikali ya mtaa na chama kama kuna kero ili iweze kutatuliwa "alisema Kudunale.

Alisema Wajumbe wa shina ambao wameshindwa kwenda na kasi ya utendaji wa kazi huo
Wakae chonjo kiti kikaliwe na mwingine.

Aidha alisema Kamati ya siasa ya Tawi la mtambani Mei  mwaka huu ina mkakati wa Kufanya   mkutano mkuu hivyo mwisho wa Mei mwaka huu kila Mjumbe afanye mkutano wake.

Alisema Kamati ya Siasa Tawi la Mtambani inatarajia kufanya ziara kila shina kuangalia uhai wa chama na Jumuiya

 Aliwataka Wajumbe wa shina kufanya kazi za chama cha Mapinduzi  na kutatua changamoto za wananchi wake.

Kudunale alisema kwa sasa CCM inaelekea katika Uchaguzi wa serikali za mitaa kama umeshindwa kufanya shughuli za chama kaa chonjo.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM TABATA Mtambani Hashimu Msekwa alisema   Tawi la CCM Tabata Mtambani muda wa kuishi kwa mazoea kwa sasa umekwisha kila mmoja anatakiwa kufanya kazi za chama.

 "Muda wa kuishi kwa mazoea kwa sasa umekwisha CCM mpya kuanzia ngazi ya MWENYEKITI wa Taifa, Katibu wote wapya hivyo kila mtu amemtaka awajibike kwa kuitendea nafasi yake  "alisema Msekwa.

Msekwa alisema kuna watu wanaomba uongozi lakini wanashindwa kuwajibika wanakuwa kama wamelazimishwa katika uongozi amewataka wapishe  ili wengine wapewe.

Alisema Jumuiya ya Wanawake UWT Tawi la Mtambani anaitegemea kuwa ni jeshi kubwa katika shughuli za chama na jumuiya zake na anashilikiana nao katika shughuli mbalimbali za chama na serikali.

Wakati huohuo Msekwa alielezea uchaguzi wa Serikali za Mtaa alisema muda Bado wale walianza kampeni watashughulikiwa kuanzia balozi wa shina.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake UWT MTAMBAN Amida Mstapha alisema shina la balozi likibainika kuna ugonjwa wa Dengue
wa kwanza kuwajibika mjumbe wa shina kwa Kuweka Mazingira machafu.


Share To:

msumbanews

Post A Comment: