Thursday, 18 April 2019

Bibi Anayetuhumiwa Kuua Mwanafunzi Auawa na Wanachi Wenye Hasira

Tukio lisilo la kawaida limetokea Wilayani Muleba Kata ya Kishanda Mkoani Kagera ambapo mtoto mwenye miaka saba Ismail Hamisi ambaye alipotea tangu April 5 akitokea shule na jana usiku amekutwa kwenye shamba la bibi mmoja akiwa amefukiwa kwenye shimo tayari ameshapoteza maisha.

Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi wa maeneo hayo kukata migomba ya bibi huyo na kumuua kwa kumchomo moto akiwa ndani ya nyumba yake

Kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amesema kuwa mtoto huyo alitoweka April 5 mwaka huu alipoondoka nyumbani kwenda shule, lakini hakuonekana tena hadi  mwili wake ulipogundulika umezikwa katika shamba la bibi huyo, akiwa na sare zake za shule.

Aidha Kamanda Revocatus amesema Taratibu za kiuchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo zinaendelea kufanyika

No comments:

Post a Comment