Thursday, 25 April 2019

Ben Pol amvisha pete ya uchumba mpenzi wakeMsanii wa muziki Bongo, Benard Paul a.k.a Ben Pol amemvisha pete ya uchumba mpenzi wake Anerlisa Muigai raia wa Kenya.

Ben ameweka wazi kuhusu hatua hiyo kupitia mtandao wa Instagram baada ya kuposti picha akiwa amepiga goti mbele ya mwanadada huyo ikiwa nikiashiria cha safari yao rasmi ya uchumba baada ya mrembo huyo kusema ndiyo.

Mkali huyo wa RnB amekuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo ambaye ni mfanyabiashara kwa kipindi kirefu sasa na miezi michache iliyopita alionekana kwenda kujitambulisha mbele ya familia ya mwanadada huyo nchini Kenya.

No comments:

Post a Comment