Waziri wa Nchi ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za mitaa, Seleman Jafo, ameagiza ndani ya siku 14 kwa Halmashauri 21 ambazo zilishindwa kuwasilisha fedha zilizotengwa kwa ajili ya lishe katika halmashauri zao kujieleza kwanini hazikufanya hivyo.

Waziri Jafo  ameagizo wakati alipokuwa akifungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala wa mikoa, waganga wakuuwa mikoa, wawakilishi toka taasisi ya chakula na wadau wa maendeleo,waliokutana kutathmini hali ya lishe hapa Nchini na mahali walipofikia katika mpango wa kwanza wa lishe wa august 2018 hapa Nchini.

Waziri Jafo amesema kuna halmashauri therathini na moja hazikutoa fedha zilizotengwa kwa ajili ya kutekeleza hali ya lishe katika maeneo hayo hali iliyosababisha kushindwa kutekelezwa kwa malengo ya lishe ndani ya halmashauri hizo.

“Ni agize ndani ya siku 14 halmashauri 21 zitoe maelezo ya kina kwa wakuu wao wa mikoa kwanini hazikutoa fedha zilizotengwa ndani ya halmashauri hizo kwa ajiri ya lishe kwanini hazikufika. Na ninyi wakuu wa mikoa baada ya siku hizo kumi na nne baada ya hapo nipate maelezo ya kwanini zilishindwa kutekeleza mikataba hiyo wakati halmashauri nyingine zaidi ya mia mija zimetekeleza” alisema Jafo

Kwa upande mwingine Waziri Jafo amekemea vikali tabia ya wakuu wa idara ambao hawafiki kwenye semina zinazohusu lishe na kuwaagiza watumishi wengine ambao hawana uelewa katika sekta hizo na kusababisha elimu hiyo kutokufikia mahala husika kwa uzembe wa wakuu wa idara hizo.
Share To:

Post A Comment: