Wednesday, 6 March 2019

UVCCM WILAYA YA RUFIJI YAWASHUKIA WANAFUNZI 20 WENYE MAZINGIRA MAGUMU KATA YA CHUMBIKamati ya Utekelezaji ya Uvccm Wilaya ya Rufiji Chini yake Comred Juma Kwangaya yawashukia wanafunzi 20 wenye Mazingira magumu.

Kamati ya utekelezaji ilitoa madaftari saba, Peni saba na rula moja kwa wanafunzi wote 20

Akikabidhi msaada huo Mwenyekiti uvccm Rufiji alisema "Uvccm wilaya ya Rufiji unawapenda sana Wanafunzi na ipo tayari kuwasaidia kwa namna yoyote ile, Tunatambua mapenzi ya dhati aliyonayo Mwenyekiti wetu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, ambae pia ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Joseph Pombe Magufuli ya kuwaletea elimu bure na sisi kama wasaidizi wake tunaotokana na chama chake tunamuunga mkono"

Mwenyekiti aliendelea kusema "Niwaombe sana musome kwa bidii kwani elimu ndio Ufunguo wa Maisha, tukisoma kwa bidii tutakuja kuwa madaktari, walimu, wabunge, na Mawaziri wa baadae"

Nae kijana mmoja aliyepata mchango huo aliwashukuru Uvccm wilaya ya Rufiji kwa msaada huo na wanaendelea kuwaombea uvccm Rufiji waendelee kujito kwa ajili ya wanafunzi mbalimbali ndani ya Rufiji.


Imetolewa na
Ritha William Monia
Katibu hamasa na chipukizi Rufiji.

No comments:

Post a Comment