Thursday, 7 March 2019

TRA yaishushia rungu Kili MarathonMamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yaishushia rungu waandaaji wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon ‘Kili Marathon’ wakitakiwa kulipa kodi ya Sh536 milioni.

Meneja wa TRA mkoa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo alikataa kuingia kwa undani kuhusu suala hilo zaidi ya kusema tayari walishawapelekea waandaaji hao, ilani ya kuwataka kulipa malimbikizo ya kodi.

Mashindano hayo huvutia wakimbiaji zaidi ya 10,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani, hufanyika kila mwezi Machi katika mji wa Moshi, na safari hii yalifanyika Machi 3.

“Mimi sipo Moshi niko Dodoma, lakini hilo jambo tulishalifanyia kazi na kuwapelekea, kwa vile na wao wamekueleza kuwa wamepata madai ya TRA basi wanatakiwa watimize wajibu wao,”alisema Mbibo.

Mmoja wa waandaji hao, John Addison alisema TRA waliwakadiria kodi kwa mwaka 2016 na 2017 ambayo inafikia Sh536 milioni kwa njia ya ilani ya dharura.

No comments:

Post a Comment