Na Mwandishi Wetu, Morogoro

Cha Mapinduzi cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimewataka wapinzani wa chama hicho kutohoji Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amerudi chama tawala kwa sababu ipi kwani hakuna asiyejua kuwa mwanachama huyo amekulia ndani ya chama hicho na kutoka kwake kwenda upinzani ilikuwa ni ajali mbaya ya kisiasa.

Kimesema ikiwa chadema viongozi wake alipotoka walimlinganisha Lowassa ni tembo wa siasa nchini ; ccm wanamuelewa Lowassa ni kati ya mibuyu miongoni mwa mibuyu minene inayotikisa katika uwanja wa siasa za Afrika Mashariki.

Hayo yameelezwa  na Katibu wa CCM Mkoa Morogoro Shaka Hamdu shaka alipoulizwa kuhusiana na kurudi kwa Lowasa huku mwenyewe akitaka asiulizwe msingi, chanzo wala sababu ya kurudi kwake kwani anadai amerudi nyumbani na kutaka wananchi kumsaidia Rais Dk John Magufuli .

Shaka alisema ni kweli huwezi kuushangaa mshale ambao chanzo chake ni mti na unaporudi porini kwani huko ndiko mahali ulikokuwa kabla ya kukatwa na kufanywa upinde uliowekwa na kipande kidogo cha chuma na kuwa silaha .

Alisema kila upinde asili yake ni mti ambao kwanza ulikatwa aidha toka kwenye msitu mkubwa au pori nene lenye aina nyingi za miti imara na lowassa ni moja kati ya miti migumu hivyo kurudi kwake kiuhalisia na kinadharia hakuhitaji kuhojiwa na yeyote au kutiliwa shaka.

"Kama Chadema walimfananisha Lowasa na tembo wa siasa kwetu ni hazina ya siasa kwa maendeleo yake ambayo haifilisiki na kurudi kwake hakupaswi kuhojiwa na mtu yeyote aidha kutoka nje au miongoni mwa wana CCM "Alisema shaka .

Aidha katibu huyo aliwataka wapinzani kuelewa na kutafakari msingi wa wanachama na viongozi wengi kurudi ndani ya ccm wakati huu ambapo chama kimekuwa na taaswira pana ya kuleta mageuzi ya kiuchumi na utekekezaji endelevu wa dhana ya maendeleo ya pamoja .

Shaka alisema mtu yeyote mwenye kupima mambo kwa ustadi anayetumia vipimo vya busara, hekima na maarifa yake hatakubali kuwa nje ya ccm au kuendelea kupingana na uongozi wa Rais Dk John Magufuli badala yake atakiri baada ya kushuhudia yanayofanyika ni mambo makubwa.

"Msimuhoji Lowasaa amerudi CCM kwa sababu gani kwani amrejea nyumbani mfano wa mshale uliorudi tena porini au kukutwa ukiwa kati kati ya msitu mnene. Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa mahiri ambao walipata ajali ya kisiasa kwa bahati mbaya bila kutarajiwa "Alisema

Alisema mtu kuendelea kupinga mambo yanayofanywa na utawala wa Rais Dk Magufuli kunahitaji ziada ya akili za kijuha na iwapo kweli akili zako zinafanya kazi kwa viwango, hutabeza yanayofanyika ambayo ni manufaa ya pamoja kimaendeleo.

Alipoulizwa ni kwasababu ipi yeye alikuwa miongoni mwa viongozi waliokuwa wakimshambulia kwa maneno makali wakati akiwa upinzani, shaka alisema watu hupopoa mti wenye mabugo ili wapate faida na hawezi kuangua matunda ambayo huwezi kuyauuza popote.

"Nilimshambulia nikijua alijikwaa na kuangukia upande usiostahili . Nilitamani azinduke na kurudi upande uliofanana na uhalisia wa maisha yake. Uchapakazi wake nilihitaji aungane na Dk Magufuli ili kuleta mabadiliko ambayo hayawezi kutokea akiwa nje ya CCM . Kurudi kwake nyumbani haitakuwa busara kuhojiwa "Alisema katibu huyo wa mkoa

Shaka ni mmoja kati ya viongozi wa ccm waliokuwa mstari wa mbele kumtupia madongo mazito kiongozi huyo wakati akiwa chadema na sasa akitaka wanaomuhoji Lowassa kwanini amerudi ccm waache kufanya hivyo ili kumuacha apumue huku Rais Magufuli akiendelea kujenga heshima ya Taifa pamoja na kurudisha umoja na mshikamano bila kujali itikadi, ghilba wa visasi kisiasa kitendo kinachonesha kuwa Rais magufuli amekomaa katika medani ya kisiasa na kiungozi.
Share To:

Post A Comment: