Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Abrahaman Kinana wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alipotembelea shule hiyo iliyokosa umeme kwa miaka 16 ambapo yeye ndiye amekwenda kuuwasha. 
Diwani wa Kata ya Muriet Fransis Mbise akimkaribisha Waziri wa Nishat Medard Kalemani katika kata hiyo, ambapo mwenyeji waje ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Gabriel Daqqaro
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akimpa zawadi mmoja wa wanafunzi katika Shule ya sekondari ya Abrahaman Kinana alipojibu swali 
Baadhi ya wananchi wa kata ya Muriet wakimsikiliza Waziru wa Nishati Medard Kalemani waliokuwa wamejikusanya waliposikia atapita maeneo yao



Na. Vero Ignatus, Arusha

Serikali imewaagiza meneja wa shirika la ugavi wa umeme nchini(TANESCO),kuhakikisha kuwa ifikapo machi 30 mwaka huu wawe
wamewaunganishia umeme wananchi wote ambao walikwisha lipia kuunganishiwa umeme kote nchini.

Waziri wa Nishati,dk.Medard Kalemani ameyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Murriet,jijini hapa alipokuwa katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini(REA)awamu ya tatu.

Alisema kuwa Wizara yake kwa muda mrefu imekuwa ikipokea malalamiko ya wananchi kutoka maeneo mbalim bali hapa nchini wakidai kuwa walikwishalipia kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu lakini hadi sasa hawajaunganishiwa jambo ambalo Wizara yake haitalivumilia.

“Katika maeneo mbalimbali ninayopita hapa nchini nimekuwa nikilalamikiwa na wananchi kwamba wamelipia kuunganishiwa umeme kwa muda mrefu lakini hadi sasa hawajaunganishiwa,hivyo nawaagiza mameneja wa mikoa wa Tanesco kote nchini kuhakikisha kuwa ifikapo machi 30 mwaka huu kila aliyelipia anaunganishiwa”alisisitiza Kalemani.

Aliwataka wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA awamu ya tatu kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ubora unaotakiwa na kuhakikisha kuwa wanakamilisha mradi kwa wakati ikiwa ni pamoja na kutoruka nyumba pindi wanapounganisha umeme huo .

Katika ziara hiyo Waziri kalemani aliwasha umeme katika shule ya sekondari Kinana na Zahanati ya Nadosoito zilizopo katika Kata ya
Murriet jijini hapa,ambapo aliwataka wananchi kuchangamkia fufsa hiyo ya kuunganishiwa umeme huo kwa shilingi 27,000 tu na kuonggeza kuwa mwananchi ataunganishiwa umeme ndani ya siku 7 tangu kulipia.

Pia Waziri Kalemani alipata fursa ya kutembelea na kukagua utendaji kazi wa baadhi ya vituo vya mafuta vya mjini hapa ambapo aliagiza kuwa
wafanyabiashara wote wa vituo vya mafuta kanda ya kaskazini wanatakiwa kuchulia mafuta katika bandari ya Tanga na sio Dar es Salaam na kwamba watakaokiuka agizo hilo la serikali watachukuliwa hatua.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Zahanati ya Nadosoito,Dk.Amina Abrahamani aliupongeza uamuzi huo wa serikali wa kuwasha umeme katika kituo hicho na kueleza kuwa itarahisha utoaji wa huduma za afya kwani hapo awali baadhi ya huduma zilikuwa hazitolewi kutokana na zahanati hiyo kutokuwa na umeme.

Katika ziara hiyo Waziri Kalemani aliambatana na watendani wakuu wa shirika la ugavi wa umeme nchini(Tanesco)Wakala wa umeme vijijini((REA) na viongozi wa serikali mkoani hapa ambapo alipata fursa ya kukagua utekelezajii wa mradi wa REA pamoja na kuzungumza na wananchi
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: