Tuesday, 5 March 2019

Serikali yapiga marufuku abiria kusafirisha vifurushi na baruaNaibu Waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye amepiga marufuku magari yote ya abiria kusafirisha vifurushi vya aina yoyote zikiwemo barua bila kuwa na leseni kutoka Mamlaka ya mawailiano nchini.

Pia ameagiza mamlaka ya kudhibiti usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA kuendesha oparesheni kali katika kudhibiti vitendo hivyo.

Naibu Waziri Nditiye ametoa agizo hilo mjini Musoma mkoani Mara wakati akizungumza na watumishi taasisi mbalimbali ambazo ziko chini ya wizara hiyo ikiwemo kampuni ya simu nchini TTCL na shirika la Posta Tanzania.

No comments:

Post a Comment