Friday, 8 March 2019

RC Mnyeti amwambia Lukuvi hakuna mgogoro wa ardhi uliotushinda Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexender Mnyeti amemwambia waziri wa Ardhi,nyumba na Maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi kwamba mkoa huo hauna mgogoro na hata siku akaija kutatua migogoro ya ardhi atamshangaa sana.

 Ameyazungumza hayo kwenye kikao cha waziri Lukuvi kilicholenga kutatua mgogoro wa muda mrefu kati ya wananchi wa mtaa wa Singu kata ya Sigino mjini Babati.

Ambapo baada ya uchunguzi kufanywa wamekubaliana kuwa wananchi 104  waliokuwa wanaishi eneo hilo wapatiwe maeneo mengine kwa ajili ya shuguli zao za kilimo pamoja na asilimia 52 ya fedha za fidia atakazolipwa mwekezaji Agric Evolution Ltd huku yeye mwekezaji akipata asilimia 48 ambayo ameiridhia mbele ya wananchi hao.

No comments:

Post a Comment