Kufutia tahadhari ya mvua kubwa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa nchini, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari ya mapema ilikukabiliana na majanga ya mafuriko huku akidrwataka wakazi wa mabondeni kuhama.

RC Makonda amesema ujenzi holela na tabia ya watu kutupa taka kwenye mifereji na mito ndio imekuwa chanzo kikubwa cha mafuriko hivyo amewahimiza wananchi kuacha mara moja tabia hiyo.

Aidha RC Makonda ametoa siku saba kwa wakala wa barabara za Mjini na Vijijini TARURA kuhakikisha wanaziba viraka katika barabara kwakuwa vimekuwa usumbufu na kero kwa watumiaji wa barabara huku akiwaagiza TANROAD kusafisha miundombinu ya Mito, mitaro na madaraja yaliyoziba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: