Friday, 8 March 2019

RC Gambo atoa onyo kali kwa wanaowarubuni wanafunzi


Serikali imesema itaendelea na jitihada zake kupambana na watu wote ambao wamekuwa wakiwarubuni na kushirikiana kwa namna moja au nyingine kuwaficha wahalifu wanowapatia mimba wanafunzi ambao wakati mwingine wamekuwa wakishirikiana na wazazi wa watoto hao.

Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ametoa onyo hilo wakati wa hafla ya kukabidhi kadi 200 za matibabu za NHIF toto afya kadi kwa niaba ya waziri wa afya zilizotolewa na benk ya Stanbic kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima wakiwemo mia moja kutoka Mkoa wa Arusha na mia moja kutoka mkoa wa Kilimanjaro.

Amesema pamoja na jitihada mbalimbali za serikali za kupambana na suala la mimba za utotoni hasa kwa wanafunzi wamekuwa wakikosa ushirikiano kutoka kwa wazazi jambo ambalo amesema serikali haitavumilia vitendo hivyo.

Kwa upande wao viongozi wa Benk ya Stanbic wamesema benki hiyo imeamua kuwasaidia watoto wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu kwa kutambua kuwa suala la afya ni muhimu katika ukuaji wa kila mtoto ambao ni taifa la kesho.

No comments:

Post a Comment