Sunday, 10 March 2019

NFRA LAZIMA INUNUE MAZAO YA KUTOSHA KWA WAKULIMA

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akishiriki shughuli za maendeleo pamoja na wananchi wakichimba msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Masangula iliyopo katika kata ya Nyimbili akiwa katika ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akikagua shamba la Kahawa lenye ukubwa wa zaidi ya Hekari 400 linalomilikiwa na Diwani wa Kata ya Nyimbili Mhe Tinson Nzunda wakati akiwa katika ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza kwenye ibada maalumu ambapo alichangia Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za ufugaji nyuki katika vikundi vya ufugaji nyuki kwenye kanisa la FPCT Ilolo sambamba na kuchangia kwaya kwa ajili ya kuendelea kuhubiri injili.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akicheza ngoma ya asili pamoja na wananchi akiwa katika ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa.
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisalimiana na wazee akiwa katika ziara ya ukaguzi na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimboni Vwawa.

Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Songwe

Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) umetakiwa kununua mahindi mengi kwa wakulima kwani kufanya hivyo kutaongeza wigo wa masoko kwa wakulima wa mazao mbalimbali ya nafaka nchini.

Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye pia ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji na kata ya Wasa vilevile katika kijiji cha Ibebwa kilichopo katika kata ya Msia akiwa katika ziara jimboni humo kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwenye miradi ya maendeleo.

Mhe Hasunga alisema kuwa NFRA inapaswa kubadili dhana ya kununua mahindi kwa ajili ya hifadhi pekee badala yake wanapaswa kununua mahindi kwa ajili ya kuyauza ili kuongeza ufanisi wa soko kwa wakulima nchini.

Katika hatua nyingine alisema kuwa tayari NFRA imeanza kutekeleza maelekezo ya serikali kwa kununua na kuuza mahindi kupitia mkataba na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) utakaopelekea kurejea sokoni kununua mahindi kwa wakulima.

Alisema NFRA pamoja na Bodi ya Nafaka na Mazao mchanganyiko zinapaswa kutekeleza wajibu wake katika ufanyaji biashara ya mazao.

Pamoja na mambo mengine Mhe Hasunga ameshiriki shughuli za Maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Sekondari Msia sambamba na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, nyumba moja ya mwalimu na matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Masangula iliyopo katika kata ya Nyimbili.

Vilevile akiwa katika ibada maalumu kwenye kanisa la FPCT Ilolo amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Mbozi kuhakikisha kuwa vikundi mbalimbali vya ufugaji nyuki vinasajiliwa.

Aidha, alichangia jumla ya Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendelezaji wa shughuli za ufugaji nyuki katika vikundi vya ufugaji nyuki kwenye kanisa la FPCT Ilolo sambamba na kuchangia kwaya kwa ajili ya kuendelea kuhubiri injili.

Aliongeza kuwa watanzania wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kufanya kazi kwa bidii huku akisisitiza kuishi katika matendo mema na kutobaguana katika shughuli za Maendeleo.

Kuhusu changamoto za upungufu wa walimu katika shule mbalimbali Waziri Hasunga alisema kuwa serikali imejipanga kutatua changamoto hizo na kwa kuanza tayari imetoa kibali cha kuajiri waalimu zaidi ya 4000 huku juhudi zingine ikiwa ni pamoja na kuwahamisha walimu kwenye shule ambazo zina walimu wa ziada.

Akiwa katika kata ya Nyimbili Mhe Hasunga amechangia Shilingi 1,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa barabara korofi ya kijiji cha Nyanyi

No comments:

Post a Comment