Marehemu Charles  Ole Ngereza enzi za uhai wake
Mwenyekiti wa Arusha Press Club (APC) Cloud Gwandu akiwa msibani nyumbani kwa marehemu Charls Ngereza na baadhi ya waandishi kama wanavyoonekana pichani. 
 Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Mkoani Arusha wakiwa msibani nyumbani kwa Marehemu Charles Ngereza eneo linalofahamika kama Kwa Mrefu.
Na. Vero Ignatus, Arusha.

Mwandishi wa habari aliyekuwa muwakilishi wa habari wa ITV na Radio one hatimae idhaa ya Kiswahili DW mkoani na makamu mwenyekiti wa Arusha Press Club Arusha Charles amefariki duania leo alfajiri

Marehemu alianza kuugua mwishoni mwa mwezi December 2018  ambapo alianza kupatiwa  matibabu katika  hospitali ya KCMC, ambapo alihamishiwa nchini India kwa matibabu zaidi na baadae alirudi nyumbani nakuendelea kujiuguza.

Hata hivyo hali yake ilibadilika ghafla hapo jana mchana na kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kisha kuhamishiwa Hospitali ya ST Elizabeth Mkaoni Arusha na kufariki dunia alifajiri ya leo

Kwa upande wake mwenyekiti wa Arusha Press Club Cloud Gwandu amesema kuwa msiba huo ni mzito kwa wanahabari wa mkoa wa Arusha kwani marehemu alikuwa ni mchapakazi, asiyekuwa mvivu na alikuwa mtu wa viwango na ubora.

Kwahiyo kama kiongozi mwenzetu tumeshirikiana nae katika mambo mengi sana hata hivi  alipoondoka kuna mradi alituunganisha na wadau wake katika APC wazaidi ya milioni 500 ambao utaleta manufaa kwa wanachama wa APC na tunaamini kwamba wadau hao hawatausitisha

Waandishi wahabari kwa pamoja Jijini Arusha wamesikitishwa kuondokewa mwenzao hivyo  ametoa pole kwa wanahabari na wote walioguswa na msiba huu. Alisema Gwandu.

Nayo familia ya Marehemu `  na wanahabari  Mkoani humu wanaendelea na maandalizi ya siku ya mazishi yatakayotangazwa baadaye.

Marehemu ameacha mke mmoja na watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wa kiume.

Bwana alitoa na Bwana ametwaa Jina lake Lihimidiwe.


Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: