Saturday, 30 March 2019

MSINGI WA MAENDELEO YA NCHI NI MAENDELEO YA KWELI KWA WANYONGE ASEMA KIKWETE


Mkakati wa kuhakikisha maendeleo yanawafikia watu wa Hali ya Chini ndiyo msingi utaowafanya Wananchi waendelee kuipenda na kuichagua Ccm. Maneno hayo ameyasema leo Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete alipokuwa anaweza jiwe la Msingi la Zahanati ya Kitongoji Cha Chahua huko mjini Chalinze mapema hivi leo.

Akiweka jiwe la Msingi , Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete alieleza furaha yake juu ya mafanikio ambao Halmashauri yake imepata kwa upande wa Afya,Elimu,Maendeleo ya Jamii na kusisitiza kuwa haya yanatokana na msimamo ambao Chama Cha Mapinduzi kinasimamia inapofika katika utekelezaji wa ilani yake ambayo inawalenga kuwapelekea Mabadiliko ya Kweli wananchi wa hali za chini kabisa.Mheshimiwa Mbunge Ridhiwani hakusita kueleza jinsi Raisi Magufuli anavyoendelea kupambana kuwasaidia Watanzania hasa katika kuwapatia huduma bora hasa kwa Upande wa Afya.

"Katika Halmashauri ya Chalinze tumejenga zaidi ya Zahanati 86 katika vitongoji na Vijiji ,Vituo vya Afya zaidi ya 13 na Sasa tunakamilisha Hospitali ya Wilaya ambayo fedha Kiasi cha Shilingi Milioni 500 zinatarajiwa kuletwa kumalizia Ujenzi pamoja na kununua vifaa tiba. Tunachopaswa wana Chalinze wenzangu ni kuendelea kuunga mkono juhudi hizo ambazo Raisi Magufuli anafanya akishirikiana nami Mbunge wenu,Diwani wetu na Mwenyekiti wetu wa Kitongoji." Mbunge Ridhiwani Kikwete alisisitiza.

“Katika Kata yetu ya Bwilingu, mambo mengi ya kimaendeleo tunayatekeleza ikiwa ni pamoja na kumalizia ahadi za Mheshimiwa Raisi alizozitoa kipindi cha kampeni. Katika Upande wa Elimu ,tunapambana kupunguza wingi wa Wanafunzi pale Shule ya sekondari ya Chalinze kwa kumalizia shule ya sekondari ya pera na mkakati mwengine wa kuanzisha ujenzi wa Shule ya sekondari ya Chahua." Mheshimiwa Mbunge pia aligusia juu ya Ujenzi wa Maabara ya Kisasa katika kituo cha Afya Chalinze ili kusaidia vipimo vya ziada vya Kiafya.

Akizungumza kabla ya Mbunge kuweka jiwe la Msingi Mwenyekiti wa Kitongoji Bwana Sadallah Maisha alimshukuru Mbunge kwa Msaada anaowasaidia Watu wa Chahua hasa katika maendeleo ya Jamanii. " Mheshimiwa Mbunge tunakushukuru kwa Kutupatia Nondo 80 na fedha taslimu Shilingi Milioni Mbili,LAki Mbili na Nusu. Pamoja nawe Halmashauri na Nguvu zetu Wananchi."

Mbunge wa Chalinze anaendelea na Ziara ya kuangalia Shughuli za Maendeleo na Utekelezaji wa Ilani katika Vijiji,Kata na Vitomgoji mbalimbali Vya Halmashauri hiyo. Katika Hali nyengine Mvua kubwa iliyonyesha kuanzia Alhamisi imeharibu Miundo mbinu katika Mji wa Chalinze na pera na Vitongoji mbalimbali.

BAADHI YA PICHA KATIKA MATUKIO TOFAUTI TOFAUTINo comments:

Post a comment