Baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa washauri wa biashara katika malengo endelevu kwa sekta binafsi wakiwa wanajadili utekelezaji wa maazimiao 17 SDGs Jijini Arusha katika ukumbi wa Naura Spring leo. Picha zote na Vero Ignatus
Mijadala katika vikundi ikiendelea katika Mkutano wa washauri w biashara katika Malengo Endelevu leo Jijini Arusha
Mratibu wa Global Compact Network Badru Juma akionyesha azimio namba 13 ambalo linahisiana na Mazingira ambapo amesema bado ibahitajika nguvu ya ziada kuhakikisha kila mtu anatunza na kulinda mazingira 
Mzee Evarist Mallya kutoka mkoani Kilimanjaro anayesimamamia mradi wa maji kwa watu maskini (WPP) akizungumza na waandishi wa habari  (hawapo pichani

Mijadala katika vikundi ikiendelea katika Mkutano wa washauri w biashara katika Malengo Endelevu leo Jijini Arusha
Pichani ni changamoto 17 duniani ambazo leo katika mkutano wa wadau wa biashara katika malengo endelevu kwa sekta binafsi ambapo leo Asasi za kiraia na Taasisi binafsi leo wamekutana kukusanya ripoti 

Na. Vero Ignatus, Arusha

Mtandao wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania unaohusu Mpango wa Maendeleo Endelevu SDGs  umefanikiwa kuzileta pamoja Asasi za kiraia  na Sekta binafsi ili kutathimini utekelezaji wa  Mpango wa Maendeleo Endelevu Tanzania

Akizungumza katika mkutano huo Mratibu UN Global Compact Badru Juma   amesema kuwa  Mwaka huu Mwezi July  Tanzania inawasilisha ripoti yao ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu kwenye mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa  

Pia amesema jitahada ambazo wamekuwa wakizifanya ili kujenga uelewa wa kutosha kuhusu Mpango wa Maendeleo  Endelevu kwa mwananchi ni kuzikutanisha pamoja sekta Binafsi na Serikali.

Amesema kuwa Majumuisho ya Pamoja ya utoaji wa Taarifa za Utekelezaji wa Mpango wa Malengo Endelevu SDGs utafanyika Mkoani Dar es salaam mwezi Julai

Mipango ya Maendele  Endelevu SDGs yapo kumi na Saba Tanzania inasimamia lengo la kwanza na la Kumi na Tatu ambayo ni kutokomeza umasikini na Mabadiliko ya Hali ya Hewa.

Afisa Mipango wa Forum Concerning Change FCC kutoka Dar es salaam Ephrasia Shayo  amesema katika kuhakikisha  Mpango wa Maendeleo Endelevu SDGs unatakelezwa katika Jamii  wamekuwa wakitoa elimu kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hali ya Hewa.  

Hata hivyo Mkurugezi wa Taasisi isiyo kuwa ya kiserikali  water for the Pour people  Mshiriki katika Mkutano huo amesema wamekuwa  wakiwasiliana na wananchi ambao hawana uwezo wa kuunganisha Maji  kwaajili ya kutafuta wafadhili  kwaajili ya kusaidia kuunganisha maji.

Amesema hadi sasa ameshawasajili watu 100 kwaajili ya mradi huo wa maji, pia ameiomba Serikali kupunguza bei ya kuunganisha maji kwani watu wenye kipato cha chini hawana uwezo wa kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwaajili ya maji. 

Mwisho
Share To:

Vukatz Blog

Post A Comment: