Mkurugenzi wa Kampuni Otterlo Bussiness Cooperation (OBC) Isaya Mollel akiwasili katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo alisomewa mashtaka kumi 10.Picha na Ferdinand
Shayo.

Na  Ferdinand Shayo,Arusha.
Mkurugenzi wa Kampuni Otterlo Bussiness Cooperation (OBC)  Isaya Mollel amesomewa mashtaka 10 ikiwemo  uhujumu uchumi ,utakatishaji wa fedha kifungu cha 12 (c) cha sheria ya utakatishaji wa fedha haramu namba 12 ya mwaka 2006,pamoja na kukwepa kodi kiasi cha shilingi bilioni 2.8  pamoja na kosa la kughushi nyaraka .
Mollel amefikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha na kusomewa mashtaka 10 na Mwendesha Mashtaka wa Serikali (DPP) Oswarld Tibabyekomya ambapo mtuhumiwa amewakilishwa na Joho la mawakili wakiongozwa na Wakili Method Kimomogolo.
Aidha Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo Niku Mwakatobe amesema kuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi hivyo kesi hiyo itatajwa tena March 18 mwaka huu.
Kaimu Mkuu wa Takukuru mkoa wa Arusha  Frida Wikesi amesema kuwa wamemshikilia mkurugenzi huyo wa OBC alishikiliwa na Takukuru na kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ambapo amesomewa  mashtaka yanayomkabili.
Frida ametoa onyo kwa Viongozi wa serikali na taasisi kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwa ni hawatasita kuwachukulia hatua.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: