Wednesday, 27 March 2019

Meya Boniface, atekeleza ahadi yake azindua viwanda viwiliMstahiki Meya Manispaa ya Ubungo Mh,Boniface Jacob; leo Amegawa msaada wa vyerehani kumi (10) Vya kisasa Vinavyogharimu kiasi cha Tsh Millioni 20 Kwa Vikundi viwili (2) Vya Wanawake Manispaa Ya Ubungo ambavyo ni  MASHUJAA WOMEN GROUP na VICTORIA FOUNDATION GROUP

Katika Hafla hiyo ya ugawaji wa Misaada hiyo ya vyerehani kumi (10) kwa lengo la Kuwawezesha Wanawake kujikwamua kiuchumi, na kuwapatia Mafunzo ya ushonaji na  Ujasiriamali

Mstahiki Meya Ameshirikiana na Kiwanda Cha Ushonaji cha  SPESHOZ TANZANIA ambapo Mkurugenzi wake Bw,Jeffrey Jessey amesema Kampuni Yake Itaunga mkono Juhudi za Mstahiki Meya za Kuwawezesha Wanamke kujikwamua Kiuchumi Kwa Kutoa Mafunzo ya Miezi mitatu(3) kwa wanawake 48 wa  Vikundi vyote viwili ( 2) Vya wakina Mama Waliopokea Misaada hiyo Kwa awamu hii ya Kwanza.

Aidha Mkurugenzi mwenza wa SPESHOZ TANZANIA Bi Cecilia  Mosha, amehaidi kuendelea kutoa Ushirikiano Kwa Mstahiki Meya katika awamu zingine zitakazo fuatia Katika Programu ya Ugawaji Vyerehani kwa ajili ya Kumsaidia Mwanamke Kujikwamua Kiuchumi, Pamoja na kutoa wito kwa Wanawake wengine kuitikia  fursa ya Mstahiki Meya na kufanyia kazi kwa Vitendo kauli ya Rais Magufuli ya Tanzania ya Viwanda
Mstahiki Meya ametoa wito kwa wakina Mama wengine ndani ya Manispaa ya Ubungo kuendelea kuandika barua za Maombi na Maandiko ya Mchanganuo ya Miradi ya Ushaonaji ,Kwa ajili ya kupatiwa Misaada Awamu zingine zinazofuata.

IMETOLEWA NA
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO
25-03-2019

No comments:

Post a Comment