Friday, 22 March 2019

MBUNIFU WA MAVAZI KUTOKA TANZANIA APEWA TUZO YA USHAWISHI NA RAIS WA MISRI ABDELFATTAH ELSISI,JIJINI ASWAN MISRI

Mbunifu wa mavazi na mwanaharakati wa vijana kutoka Tanzania Rahma Bajun alipokea  tuzo ya utambuzi kutoka kwa Rais wa Misri Abdelfattah Elsisi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki.

 

Tuzo hiyo ilitolewa jijini Aswan nchini Misri kwenye mkutano wa “Arab and African Youth Platform” uliofanyika hivi karibuni Rahma sambamba na vijana wengine 9 kutoka nchi za Afrika na za Kiarabu wanaotoka kwene sekta mbalimbali wamepokea tuzo hizo za heshimwa kwa mchango wanaotoka vijana, nchi zao na Afrika kwa ujumla.
Rais wa Misri Abdelfattah Elsisi(Kushoto) akimkabidhi Mtanzania Bi. Rahma Bajun tuzo ya 'Most inspiring youth in Africa and Arab region' wakati wa mkutano wa Arab and African Youth Platform uliofanyika nchini Misri.
Mbunifu wa mavazi na mwanaharakati wa vijana kutoka Tanzania Rahma Bajun (wa tatu kutoka kushoto) akiwa pamoja na washiriki wengine kutoka Barani Africa wakati wa mkutano huo.No comments:

Post a comment