Friday, 8 March 2019

Mbunge ANATROPIA awapa mafunzo Wanawake 300 wajasirimaliNa Heri Shaban
MBUNGE wa Viti maalum Wanawake Manispaa Ilala ANATROPIA Theonest amewapa mafunzo kwa vitendo Wanawake  300 wa Manispaa hiyo bure .

Mafunzo hayo ya Wanawake 300 yalifanyika mwishoni mwa wiki kata ya Kiwalani yalishirikisha Wanawake mbalimbali pamoja na Wanaume wasio kuwa na ajira.


Akizungumza mara baada kumaliza mafunzo hayo Anatropia alisema dhumuni la mafunzo hayo kila Mjasiriamali wa Wilaya Ilala aweze kupata ujuzi wake akimaliza kujifunza akafungue Kiwanda chake na  kukuza uchumi wa Viwanda katika kuunga mkono juhudi za Serikali

" Ofisi yangu ya Mbunge wa Viti maalum Manispaa
Ilala ipo TABATA Barakuda Leo imewapa mafunzo kwa vitendo Wajasiriamali mbalimbali ili waweze kuunda viwanda vyao  naamini kila mtu aliyepata mafunzo hayo atafungua kiwanda "alisema ANATROPIA.

Anatropia alisema mafunzo hayo yameshirikisha kata sita za Manispaa ya Ilala kujifunza utengezaji Batiki, ushonaji,pamoja na Wajasiriamali ..

Aliwataka Wajasiriamali wote wsliopata mafunzo watumie elimu hiyo  katika kutafuta fursa na kukuza Masoko.

Kwa upande wake Mwalimu aliyekuwa akitoa mafunzo Mkurugenzi wa Majani Mery Majani alisema Washiriki wamepongeza juhudi za mbunge za kuwapatia mafunzo bure, amewataka Wajasiriamali wengine zinapotokea fursa kama hizo Washiriki     watumie nafasi hiyo katika kujiongezea mahalifa.

Naye Mjasiriamali Charles Mkopa kutoka makundi ya vijana Ilala aliwatala Vijana Wasilalamike  na kuweka masilahi Mbele badala yale
Zinazotokea fursa watumie.

Aliwataka vijana watafute fursa waache kulalamika mitaani kwa kuitupia lawama serikali.

No comments:

Post a Comment