Thursday, 21 March 2019

Manispaa ya Ilala yazindua oparesheni ya ukaguzi wasiolipa leseniNA HERI SHAABAN

MANISPAA ya Ilala  Dar es Salaam wameanza oparesheni endelevu ya ukaguzi wa Wafanyabiashara wasiolipa leseni za Biashara.

Oparesheni hiyo ya kukusanya mapato ya serikali inaongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa Ilala Jumanne Shauri na Watendaji wa manispaa hiyo.

Dhumuni la ziara hiyo kukusanya  fedha  za serikali kufuatia baadhi ya Wafanyabiashara wengine sio waminifu wanashindwa kulipa leseni zao wa wakati.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam  Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jumanne Shauri alisema uzinduzi huo rasmi umeanza leo kwa ukaguzi wa Viwanda Barabara ya Nyerere na Wafanyabiashara wa Kati.

"Leo (jana) tumezindua rasmi oparesheni ya ukaguzi wa leseni pamoja na tozo ya kodi ya huduma service Levy sambamba na kuwapa elimu ya kulipa tozo ya huduma ya kodi service Levy katika zoezi hilo mtaa mmoja tumefanikiwa kukusanya shilingi milioni 12"alisema shauri .

Alisema Manispaa Ilala wamejipanga na timu yake katika kufatilia  wadaiwa sugu wa leseni ambapo wakifika wanawapa elimu kwa wale wasiolipa na kuwapa maelekezo  ya kwenda ofisi ya Halmashauri kulipa.

Wakati huohuo Shauri kumpongeza RAIS John Magufuli kwa utekelezaji wake wa miradi ya Serikali sehemu kama sehemu ya utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi CCM.

Aidha aliwataka Wafanyabiashara walipe kwa wakati watii Sheria bila shurutishwa fedha hizo wanazolipa serikali zinatumika katika huduma mbalimbali za maendeleo ikiwemo katika huduma za jamii.


Shauri alisema mara baada uzinduzi huo Aprili Mosi mwaka huu Timu yote itaingia mtaani katika ukusanyaji wa mapato ya serikali  mwaka huu tuweze kufikia malengo.

Aliwataka wananchi kutumia kipindi hichi kwenda halmashauri ya Ilala jengo la Arnatogluo kulipa kwa ajili ya kuondoa usumbufu.
Mwisho

No comments:

Post a comment