Monday, 1 April 2019

MAHAFALI YA 35 YA CHUO KIKUU HURIA YAFANYIKA KATIKA KITUO CHA ARUSHA

 Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro akizungumza kwenye mahafali ya 35 katika chuo Kikuu Huria Jijini Arusha, kushoto kwake ni makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu
Naadhibya wahitimu wa Chuo Kikuu huria Kituo cha Arusha kama wakiwa kwenye magafali
Bi Joyce Bendera akipokea cheti kutoka kwa mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Gabriel Daqqaro mara baada ya kuhitimu masomo yake kagika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
 Ndugu Godfrey Mmassy Kipokea cheti mara baada ya kuhitimu masomo yake ya elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) katika chuo kikuu huria kituo cha Arusha. 
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ya 35 ya Chuo kikuu huria Kituo cha Arusha, mkuu wa wilaya ya Arusha mjini Mhe. Gabriel Daqqaro, viongozi wa juu wa chuo kikuu huria, na viongozi wa serikali ya wanafunzi, pamoja na mwenyekiti wa chama ctawala mkoa wa Arusha Aloota Sanare. 

Na. Vero Ignatus, Arusha. 

Katika kufanikisha ujenzi wa Tanzania ya viwanda wasomi wametakiwa kutumia elimu yao kuweza vizuri kwa kuweza kujiajiri na kutoa fursa kwa watu wengine kuliko kutegemea kuajiliwa hali inayosababisha kuendelea kuzorota kwa uchumi wa nchi 

Hayo yamebainishwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro kwenye mahafali ya Chuo Kikuu Huria Tanzania tawi la arusha ambapo amewasisitiza wahitimu hao kuweza kuenda kulitumikia taifa lao kwa weredi utakao lisogeza taifa katika uchumi wa kati

Pamoja na hayo makamu mkuu wa chuo hicho kwa tawi la Arusha Marcel Masalu amesema wanafunzi waliohitimu masomo yao mwaka 2017/18 ni 145 kwa Arusha peke yake. 

 Masalu amesema Chuo hicho ndicho pekee cha Elimu ya juu Tanzania kinachotoa kozi kwa njia ya Cheti, Estashahada, Stashahada, Shahada za uzamili (Masters) na Uzamili PHD kwa njia ya masafa. 

Aidha mewataka wahitimu hao kuweza kukitangaza chuo hicho huko wanapokwenda kwa kufanya kazi zao kwa ufasaha 

Kwa upande wawanafunzi hao waliohitimu wameeleza changamoto wanazozipata ikiwa nipamoja na upungufu wa madarasa pamoja na majengo ya walimu hali inayosababisha mrundikano wawanafunzi wengi.

Nae Ndugu Godfrey Mmassy aliyehitimu  elimu yake ya Master of monitoring and Evaluation (M&E) amesema mtu yeyote akiamua kusoma akiwa kazini inawezekana kabisa ni maamuzi ya mtu binafsi

No comments:

Post a comment