Afisa Mtendaji wa Kata ya Segera wilayani Handeni Rukia Chizinga akizungumza wakati wa mdahalo wa elimu uliendeshwa kwenye shule ya Msingi Michungwani na Asasi ya Tree of Hope chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.
 Diwani wa Kata ya Segera (CCMI Akizungumza katika mdahalo huo

Mratibu wa Mradi wa Uhamasishaji na Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Halmashauri ya Handeni Goodluck Malilo akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo

 Mwenzashaji Wakili Mazule akisisitiza jambo wakati wa mdahalo huo
 Sehemu ya washiriki wa mdahalo huo wakifuatilia kwa umakini
Picha ya Pamoija
MADEREVA wa malori na madalali kata ya Segera wilayani Handeni mkoani Tanga ambao watakutwa na watoto wakiwa wanapakia machungwa watakamatwa na kufunguliwa mashtaka ya kuwafanyisha kazi ikiwemo kupelekwa mahakamani

Hayo yalisemwa na Afisa Mtendaji wa Kata ya Segera wilayani Handeni Rukia Chizinga wakati wa mdahalo wa elimu uliendeshwa kwenye shule ya Msingi Michungwani na Asasi ya Tree of Hope chini ya ufadhili wa Shirika la Foundation for Civil Society.

Alisema kama madalali na madareva wanakwenda kupakia machungwa lazima wahakikishe hawachukui watoto chini ya miaka kumi na nane haijalishi anasoma au hasomi ili mradi wapo chini ya umri huo watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

“Niwaambie madereva wa malori na madalali kwamba yoyote tukaye mkuta na mtoto…Dereva tutamfungulia mashtaka ya kumfanyisha mtoto kazi na kumpeleka mahakamani zamani tulikuwa tunaishi Polisi wanalipa faini lakini pia wazazi walikuwa wanachukuliwa hatua ila kwa sasa tutawafikisha mahakamani”Alisema Afisa Mtendaji huyo

Aidha alisema ili madereva hao na madalali waendelee kuwa salama wakati wa ufanyaji shughuli zao wakati wa kupachia machungwa wahakikishe watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane hawahusiki kwenye kazi hizo.

Naye kwea upande wake, Mratibu wa Mradi wa Uhamasishaji na Uwajibikaji wa Jamii na Mamlaka zinazohusika katika kuboresha huduma za elimu katika Halmashauri ya Handeni Goodluck Malilo alisema
 katika awamu ya pili ya mradi huo wataangalia namna ya ule wa awali ulivyoleta mabadiliko makubwa kwenye jamii husika ikiwemo hali halisi ilivyo kwa sasa na kipindi kilichopita hususani kwenye mambo waliokuwa wakiyaainisha kwenye midahalo yao.

“Wataangalia suala la uwazi na uwajibikaji ikiwemo shule kuwa na ubao wa matangazo,tatizo la utoro,changamoto za mimba na upatikaji wa chakula,Uendeleshwani wa miradi iliyokwama kwenye ngazi ya shule “Alisema .

Aidha pia alisema wakati wakianza kutekeleza mradi huo kwenye kata ya Segera wilayani humo kulikuwa na changamoto kubwa sana na utoro kwa wanafunzi ambao walikuwa wakiacha kwenda shule na kwenda kupakia machungwa kwenye malori lakini kwa sasa jambo hilo limepungua kwa kiasi kikubwa.
Share To:

Post A Comment: