Wednesday, 6 March 2019

Madereva Magari Ya Watalii Wanaoshuka Kreta Ngorongoro Wapewa Tahadhari


MADEREVA wa magari ya watalii wanaotembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro(NCAA), hususani wanaotelemka Kreta wametakiwa kuchukua tahadhari kubwa kutokana na barabara hiyo kufanyiwa matengenezo. 

Akizungumzia matengenezo hayo Kamishna wa Uhifadhi NCAA Dk. Fredy Manongi alisema, barabara inayoshuka Kreta kwa sasa imekwanguliwa ili kuifanyia matengenezo ya muda mfupi na mrefu.

“Ile barabara tumeanza mpango wa kuijenga kama barabara ile ya kupandia kutoka Kreta, kwa sasa imefukuliwa pamoja na kuwapo mashine njiani. 

“Kwa mvua hizi zinaendelea kunyesha tunawaomba madereva wawe waangalifu kwani barabara si imara,” alisema Dk. Manongi. 

Mbali ya barabara hiyo Dk. Manongi alibainisha pia barabara nyingine inayoanzia lango kuu la NCAA mpaka goloni ulipo mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nayo itaanza kujengwa kwa kiwango cha tabaka gulu la Zege. 

“Tupo tayari kuhakikisha tunawaondolea kero watalii, wamiliki wa magari ya watalii lakini pia hata sisi Mamlaka kwani tunatumia fedha nyingi kukarabati barabara ya changarawe kila mwaka,” alisema Kamishna wa Uhifadhi Dk. Manongi.

No comments:

Post a Comment