Saturday, 9 March 2019

LOWASSA ALIVYOPOKELEWA KWA KISHINDO MONDULIWaziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akipunga mkono kusalimia wanachama wa CCM Wilaya Monduli mkoani  Arusha baada ya kurejea rasmi ndani ya chama hicho.
 
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa akizungumza leo mara baada ya kupokelewa rasmi Ccm Monduli, kushoto kwake ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Loata Sanare, kulia kwake ni Katibu wa Itikadi nauenezi CCM Taifa Humphrey Polepole. Picha na habari na Vero Ignatus
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisalimiana na Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Magharibi, Godluck Ole Medeye mkono baada ya kuwasili Uwanja wa Arusha jana baada ya kurejea rasmi ndani ya CCM Monduli  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akisalimiana na Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Singida, Paraseko Kone baada ya ya Lowasaa kurejea rasmi ndani ya CCM Monduli.

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akiapa kuwa mwachama mtiifu wa CCM huku akiwa ameshika kadi ya chama hicho baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole.
Mbunge wa Simanjiro, James Ole Miliya akizungumza  wakati baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kurejea rasmi ndani ya CCM Monduli. 

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, akizungumza na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ,baada ya kurejea ndani ya chama hicho Monduli mkoani  Arusha.

Katibu wa Itikadi na uenezi Taifa Humphrey Polepole, Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa na Mwenyekiti wa CCM mkoa Alota Sanare wakiwa wameshikana mkono kama ishara ya Umoja
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa akisalimiana na wanachama wa Ccm waliofurika katika ofisi ya CCM wilaya ya Monduli leo
Lowasa akiwapungia wanachama wenzake wa CCM leo
Wanachama wa CCM wakiwa katika uwanja wa Ofisi ya CCM wilaya ya Monduli leo.

Katibu wa Itikadi na uenezi Huphrey Polepole akizungumza katika uwanja wa ofisi za CCM wilaya ya Monduli mkoani Arusha leo.
Baadhi ya wanachama wa CCM waliofurika katika ofisi,za CCM wilaya ya Monduli leo
Mbunge wa CCM wilaya ya Monduli Julius Kalanga akishuhudia tukio la kurudi rasmi CCM na kukabidhiwa kadi ya uanachama katika ofisi ya CCM wilaya ya Monduli


Na. Vero Ignatus, Monduli

Aliyekuwa waziri mkuu wa zamani Edward Lowasa amepokelewa Leo rasmi kurudi katika chama cha mapinduzi na mwenyekiti wa katibu wa itikadi nauenezi wa chama hicho Humphrey Polepole

Akizungumza mara baada ya kukaribishwa rasmi Lowassa amewashukuru watanzania milioni 6 waliompigia kura mwaka 2015 na kuwaomba kura hizo waje kumpa rais Magufuli

Amesema kuwa ameamua kurudi Ccm kwa kuvutiwa na kazi anazozifanya Dkt. Magufuli hivyo amewasihi wana monduli kumuunga mkono kwa kazi anazozifanya kwa maendeleo ya Taifa la Tanzania

'' Nimerudi nyumbani, sina maneno mengi ila nasema nimerudi nyumbani, Chadema nawashikuru sana neno langu kuu nasema nawashukuru, msinilishe maneno mdomoni"alisema Lowassa

Lowassa amesema kuwa wananchi wa Tanzania wanathamini sana Amani nakuwataka watanzania wasisikilize maneno ya kibaguzi bali wailinde Amani iliyopo kwani jambo la msingi

'' Mwalimu nyerere aliwahi kuhutubia halmashauri kuu ya ccm Taifa na kutueleza kuwa kuna viongozi wa aina mbili ambapo ni bookkikeeper na visionary leader '' alisema Lowassa, Amesema kuwa visionary leader ni kiongozi anayetazama miaka 50 ijayo atafanya vitu gani '' Nimekuwa nikisikia maneno ya kibaguzi kwamba mtu akienda kwa Lowassa anapelekwa jina kwa mkuu wa wilaya achaneni na hayo maneno hayana ukweli tuoendane, mwuislamu ampende mkristo ili amani iendelee''. Alisema

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Loata Sanare amesema kuwa wote waliokwenda upande wa pili wa upinzani wakitaka kurudi lazima wafuate utaratibu kama Lowassa kwani Lowasa licha ya kupokelewa na mwenyekiti wa ccm Taifa aliandika barua kwenye tawi.

'' Wote ambao mnataka kurudi ombeni kwa kufuata utaratibu, Wengi wenu mmevaaa nguo za ccm lakini siyo wanachama bali ni washabiki wa ccm"

Amesema kuwa wanamkaribisha nyumbani mhe. Lowasa ila wangemshangaa kama aangeendelea kubaki kwenye kundi la ajabu ajabu, Kwa upande wake Katibu wa Itikadi na uenezi CCM Huphrey Polepole amesema kitendo alichokifanya kuwa Mhe. Lowassa ni cha ukomavu wa kisiasa ametangaza tutangulize mbele maslahi ya Taifa na kuilinda Amani ya nchi

POLEPOLE amesema kuwa Lowassa amefuata taratibu zote za chama cha mapinduzi hivyo wamejadili na kuona anafaa kurudi CCM bila kuleta madahara katika chama hicho,Sambamba na hayo wanachama wengi waliokuwa chadema wamerudisha kadi zao na kujiunga na CCM ambap0 Ikumbukwe kuwa Lowasa alijiunga Chadema 2015 na kuchaguliwa kuwa mgombea wa Urais wa chama hicho na machi mosi 2019 alirudi rasmi CCM 

No comments:

Post a Comment