Saturday, 9 March 2019

LOWASA ATAJA SIRI ILIYOMRUDISHA (CCM)

Kutoka Monduli (ARUSHA)
Katibu wa Itikadi,siasa na uenezi Humphrey Polepole amewaongoza mamia ya wananchi viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) katika hafla ya kumpokea Waziri mkuu mstaafu wa awamu ya nne Edward Lowasa Wilayani monduli Mkoani Arusha.
Katika hafla hiyo Polepole amesema Chama Cha mapinduzi ni chama kinacho zitangatia sheria na taratibu za chama katika mambo mbalimbali kwa maslahi ya wananchi na ndani na nje ya CCM.
"Nilazima kufata taratibu zote za kisheria kwa mujibu wa katiba ya CCM kwa yeyote atakae jiunga na chama Cha mapinduzi ili kuweza kuendeleza Maendeleo ya nchi vinginevyo hatuta mpokea Wala kumruhusu mtu kujiunga na CCM"alisema Polepole.
Muda mchache baadae Mara baada ya kila kiapo Pamoja na wanachama wapya walio jiunga na chama tawala nchini Tanzania (CCM) Waziri mkuu mstaafu Edwad Lowasa akatumia halfa hiyo kuwataka watanzania kudumisha amani na ushirikiano chanya kwa maslahi ya Taifa ili kuendana na Kasi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Amesema ameamua kuridi CCM Kutokana na kazi, juhudi kubwa na uzalendo unaofanywa na Rais Magufuli hivyo ni wakati muafaka kuunga mkono juhudi hizo ili kusukuma gurudumu la Maendeleo mbele kwa ushirikiano na serikali ya awamu ya tano.
"Nimeamua kurudi nyumbani Sina sababu zaudi ya kusema Kuwa nimerudi nyumbani, nashukuru Sana (CHADEMA) nimejifunza mengi sana" alisema Lowasa.
Msumba news imepata Fursa ya kuzungumza na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Monduli akiwemo mwenyekiti wa viongozi wa kimila maarufu laigwanani Bw:Kisongo ole meijo na Ole Kalanga kitutu ambapo wamesema ujio wa Lowasa ni faraja na furaha kwa wakazi wa monduli kwa ujumla ili kuchochea Maendeleo katika Wilaya hiyo.
Ole meijo amesema kwa muda mrefu kumekucha na matabaka katika jamii ya wafugaji suala ambalo limekuwa chanzo Cha baadhi ya migogoro na kuduma Maendeleo hivyo wanategemea mazuri kwa ushirikiano na serikali ya watanzania.
"Lowasa atatuunganisha vyema na Rais Magufuli kwa ajili ya utatuzi wa kero ya maji kwa muda mrefu tunaamini Mambo yataenda sawa".
Lowasa amepokelewa na viongozi wa chama hivi karibuni Mara baada ya kukihama chama Cha CCM nyakati za Uchaguzi mkuu 2015 na kuelekea (CHADEMA) huku akiwa ameongoza Jimbo la Monduli kwa zaudi ya Miaka 24 kwa tiketi ya chama Cha mapinduzi CCM.

No comments:

Post a Comment